Abdul Nondo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 520
- 2,930
Ushauri wangu kwa viongozi wa serikali na mamlaka ya serikali walione hili.
Mimi najiuliza kwanini sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge wa uhuru zifungamanishwe na siku ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa tar 14 Oktoba? Mimi nashauri hizi siku zitenganishwe sababu sherehe ya mwenge inafunika(overlap) madhumuni na Maana ya siku ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa.
Inawezekana walioamua kuzifungamanisha walikuwa na nia njema ila sasa inaonekana kabisa haileti matokeo mazuri kwani kimoja kinaonekana kufunika kingine ambalo nafikiri halikuwa lengo lake. Sasa ni muda wa kutenganisha haya matukio mawili ili siku ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ibaki na uzito wake.
Angalia sherehe ya Jana tar 14 Oktoba kuanzia maudhui na yote yaliyokuwa yanazungumzwa ni mwenge na miradi na magazeti ya leo ni Mwenge na miradi sio vibaya lakini tukio la kuzima mwenge linaweza pangiwa siku yake.Kuacha hivi inafanya waandaaji na tukio zima litawaliwe na maudhui ya mwenge kuliko kumbukumbu ya Baba wa Taifa (Overlapping).
Baba wa Taifa ana mambo mengi ambayo siku ya kumbukumbu yake yanapaswa kusikika,ili kama vijana, viongozi wananchi na nchi kwa ujumla tuendelee kumuenzi katika matendo na falsafa zake nzuri kwa ajili ya nchi yetu.
Hoja ya kwamba matukio haya au siku hizi zikitenganishwa itaongeza gharama sio hoja, wala haitoongeza gharama, kumuenzi Baba wa Taifa sio lazima kutumia fedha za umma katika kumuenzi. Hayo ni mambo ambayo binafsi hata yeye alikuwa hapendi, tunaweza kumuenzi kwa namna tofauti kuipa uzito siku hiyo ya tar 14 ikawa siku ya mapumziko, vyombo vya habari vitoe historia na hotuba za Baba wa Taifa ,iwe ni siku ya wanaoweza kwenda kuzuru kaburi lake waende na Kutembelea familia yake hata pia Kutembelea makumbusho ya Mwalimu Nyerere ili kujifunza,watu kumuombea kwa imani ya dini zao.
Viongozi walioishi na Baba wa Taifa na wanaomjua watoe historia na walivyomfahamu Baba wa Taifa.Iwe ni siku ya majadiliano sehemu mbalimbali na maeneo mbalimbali juu ya historia ya Mwalimu,fikra , Mawazo na falsafa zake katika uongozi,siasa na maendeleo ili angalau tupate kujifunza na kuishi kwa matendo juu ya fikra na falsafa ya Baba wa Taifa.
Bado leo hii kuna Wazee ambao wapo hai wanaweza kutumia siku hii kumuelezea Mwalimu akina Mzee Warioba, Mzee Butiku ,Mzee wetu Balozi Charles Asilia Sanga na wengine ili iwe ni siku ya kusikia,kutafakari , kujifunza na kujitathimini kama nchi juu ya Taifa letu ,falsafa ya Mwalimu,fikra na Mawazo yake namna gani bado tunayaishi kwa vitendo .
Ili kumuenzi Baba wa Taifa vyema,na maana, lengo, dhamira ya siku ya kumbukumbu yake kuonekana kuna haja ya kutenganisha haya matukio au siku zikawa tofauti. Siku ya kuzima mwenge ijitegemee iwe na siku yake ili siku ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere tar 14 Oktoba ibaki na uzito wake.
Naomba viongozi wa serikali Mh.Rais @samia_suluhu_hassan na viongozi wengine naomba mtumie busara zenu kama viongozi kutenganisha hizi siku ili kila siku ipate uzito wake unao stahili.
Yani kuna namna nzuri ya kuifanya hii siku kwa kuipa uzito wake mkubwa bila hata kuingia gharama kubwa za serikali na siku ikawa ni hii ambayo haingiliwi au kufunikwa na tukio lingine kama ilivyo sasa inafunikwa na kilele cha kuzima mwenge.Hivyo kupoteza maana, malengo na madhumuni ya siku ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.
Kama serikali inaona haiwezekani kutenganisha matukio haya mawili ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na kilele cha kuzima Mwenge,vyema basi lengo la kuunganisha siku hii lionekane , maudhui ya siku hii yasilalie upande mmoja na kusahau upande mwingine kama ilivyokuwa Jana tar 14 Oktoba maudhui yalikuwa mwenge na miradi , magazeti karibu yote leo ni mwenge na miradi na maudhui kuhusu kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere yakawekwa kando jambo ambalo ni hatari.
Lakini pia kama serikali bado inaona haja ya kufungamanisha matukio haya mawili ni vyema sasa itangazwe rasmi miaka yote kilele cha kuzima mwenge kifanyike Kagera (Musoma -Butiama ) miaka yote iwe hivyo ili kufangamanisha matukio haya mawili kwa siku moja.
Tusipochukua hatua za haraka katika hili, Siku za usoni tutajikuta kumbukumbu za siku ya Mwalimu Nyerere inafutika na kupoteza maana.
Na kizazi kijacho ambao wengi sasa ni vijana wengi hatukuwahi kupata kuonja uongozi wa Mwalimu Nyerere, na wengi hata hawakumuona Mwalimu Nyerere,wengi wanamsikia na kumsoma. Tusipoendelea kutoa elimu, historia, kumbukumbu juu ya fikra, falsafa na Mawazo ya Mwalimu katika siasa, uongozi, maendeleo na mambo mengine hakika mnatengeneza mwanya wa kizazi hiki kumsahau Mwalimu Nyerere.
Kama waliofanya kazi na Mwalimu wapo hai Sasa, walioishi na Mwalimu wapo hai Sasa na wengine ni viongozi ndani ya serikali mnafubaza siku ya kumbukumbu ya Mwalimu namna hii, vipi kwa kizazi kinachofuata baada yenu?
Ahsante,
Abdul Nondo.
Mwenyekiti wa Ngome ya vijana ACT Wazalendo Taifa.