Siku ya Kupinga Adhabu ya Kifo Duniani - LHRC Kuadhimisha na Jukwaa la Wahariri (TEF)

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi

Tarehe 10 ya October kila mwaka, ni siku ya Kimataifa ya Kupinga Adhabu ya Kifo Duniani.

Kwa Tanzania kwa mwaka huu, Kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu Tanzania, LHRC kinazungumza na Wahariri wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, TEF, katika ukumbi wa hoteli hii ya Holiday Inn ya hapa jijini Dar es Salaam.

Mimi mwana JF mwenzako ambaye ni mwandishi wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea, ambaye pia ni mtetezi mkubwa wa haki za binaadamu na haki ya kuishi, niko hapa ukumbini kukuletea kile kinachoendelea hapa.

Wakati ukisubiria hii shughuli hapa ianze, karibu nyuzi zangu hizi uanze refreshing
Hii event iko live kwenye
View: https://www.youtube.com/live/74qsu__92pM?si=_9Et_u9v2jIC2aN_

Na hapa
View: https://www.youtube.com/live/oJDwqRmsSPE?si=ueIE-gkjwkNpFwPb

Karibu

Paskali
 
Wanabodi

Tarehe 10 ya October kila mwaka, ni siku ya Kimataifa ya Kupinga Adhabu ya Kifo Duniani.

Kwa Tanzania kwa mwaka huu, Kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu Tanzania, LHRC kinazungumza na Wahariri wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, TEF, katika ukumbi wa hoteli hii ya Holiday Inn ya hapa jijini Dar es Salaam.

Mimi mwana jf mwenzako ambaye ni mwandishi wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea, ambaye pia ni mtetezi mkubwa wa haki za binaadamu na haki ya kuishi, niko hapa ukumbini kukuletea kile kinachoendelea hapa.

Siku hizi jukwaa la wahariri limekuwa jukwaa la machawa baada uongozi wake kuonyeshwa asali
 
Shughuli imeanza kwa utambulisho wa tuliopo
Mwezeshaji kutoka LHRC ametambulisha ibara ya 14 ya katiba ya Tanzania yenye kutoa haki ya kuishi.
Katiba ndio sheria mama, sheria nyingine yoyote ikikinzana na katiba, sheria hiyo nyingine inakuwa ni batili.
Hivyo hukumu ya kifo ni batili.
P
 
Wanabodi

Tarehe 10 ya October kila mwaka, ni siku ya Kimataifa ya Kupinga Adhabu ya Kifo Duniani.

Kwa Tanzania kwa mwaka huu, Kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu Tanzania, LHRC kinazungumza na Wahariri wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, TEF, katika ukumbi wa hoteli hii ya Holiday Inn ya hapa jijini Dar es Salaam.

Mimi mwana jf mwenzako ambaye ni mwandishi wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea, ambaye pia ni mtetezi mkubwa wa haki za binaadamu na haki ya kuishi, niko hapa ukumbini kukuletea kile kinachoendelea hapa.

Wakati ukisubiria hii shughuli hapa ianze, karibu nyuzi zangu hizi uanze refreshing

Karibu

Paskali
Mnanikumbusha wanao pigwa risasi mchana kweupe, wanaotekwa na watekaji wanao jitambulisha kama wao ni mapolisi tena wanakuwa na pingu, baada ya kutekwa wanakutwa wameuawa halafu kimyaaa utadhani hakuna kilicho tokea

Only crossing our fingers will not help. Kutegemea miujiza ya Mungu na maombi haitoshi hata hivyo Mungu yuko busy sana, hili liko ndani ya uwezo wa jamii, yaani hata mbio hatuwezi kuwakimbiza ama fimbo hatuwezi kuzitafuta?
 
Mkurugenzi wa LHRC , Anna Henga, anatambulisha wageni, kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria, na mtu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria.
Pia ametambulisha wageni kutoka mtandao wa kupinga adhabu ya kifo Tanzania Chesp
Henga amesema juzi kati alikuwa Philadelphia nchini Marekani ambako nako wanajadili kuifuta nchini kwao.
p
 
Wanabodi

Tarehe 10 ya October kila mwaka, ni siku ya Kimataifa ya Kupinga Adhabu ya Kifo Duniani.

Kwa Tanzania kwa mwaka huu, Kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu Tanzania, LHRC kinazungumza na Wahariri wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, TEF, katika ukumbi wa hoteli hii ya Holiday Inn ya hapa jijini Dar es Salaam.

Mimi mwana jf mwenzako ambaye ni mwandishi wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea, ambaye pia ni mtetezi mkubwa wa haki za binaadamu na haki ya kuishi, niko hapa ukumbini kukuletea kile kinachoendelea hapa.

Wakati ukisubiria hii shughuli hapa ianze, karibu nyuzi zangu hizi uanze refreshing

Karibu

Paskali
Kituo cha sheria na haki za binadamu kilipoteza hazi yake muda mrefu sana!
 
Henga amesema kwa Tanzania adhabu ya kifo, ni kwa makosa mawili ya kuua murder, na treason, adhabu ya kifo kwa Tanzania hutekelezwa kwa kuhukumiwa kunyongwa mpaka ufe, pia kuna makoso ya kijeshi ya usaliti adhabu yake pia ni kifo kwa firing squad. Makosa hayo ya kijeshi ni siri za kijeshi.

P
 
Anna Henga, amesema, kwa mara ya mwisho, adhabu ya kifo hapa nchini ilitekelezwa mwaka 1994 enzi za utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi, Rais Mkapa, Rais Kikwete, Rais Magufuli, hawakuwahi kusaini hati yoyote ya kifo, yaani death warrant, hivyo hukumu hii haijatekelezwa kwa miaka 30!.
Kama adhabu hii haitekelezwi, tunaiacha ya nini?.

P
 
Mkurugenzi wa LHRC , Anna Henga, anatambulisha wageni, kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria, na mtu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria.
Pia ametambulisha wageni kutoka mtandao wa kupinga adhabu ya kifo Tanzania Chesp
Henga amesema juzi kati alikuwa Philadelphia nchini Marekani ambako nako wanajadili kuifuta nchini kwao.
p
Kwetu sisi wajadili kuhusu watu kutekwa, kupotezwa kinachofuata baada ya kupotezwa ni kuokotwa baada ya kutupwa ama kupatikana kwa kudra ya mwenyezi Mungu, wengine hakuna taarifa

Wajadili nini kifanyike na hatua zipi za kuchukua endapo maazimio hayo hayatatekelezwa vinginevyo hakuna umuhimu wa maadhimisho hayo hapo mwakani, wajiwekeke utekelezaji wa muda mfupi, muda mrefu na kupima malengo waliojiwekea , "monitoring and evaluation"
 
Henga amesema kwa Tanzania adhabu ya kifo, ni kwa makosa mawili ya kuua murder, na treason, adhabu ya kifo kwa Tanzania hutekelezwa kwa kuhukumiwa kunyongwa mpaka ufe, pia kuna makoso ya kijeshi ya usaliti adhabu yake pia ni kifo kwa firing squad. Makosa hayo ya kijeshi ni siri za kijeshi.

P
Mwambie henga huku uraiani
Kuna watu wana vibali vya kuua

Ova
 
Wanabodi

Tarehe 10 ya October kila mwaka, ni siku ya Kimataifa ya Kupinga Adhabu ya Kifo Duniani.

Kwa Tanzania kwa mwaka huu, Kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu Tanzania, LHRC kinazungumza na Wahariri wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, TEF, katika ukumbi wa hoteli hii ya Holiday Inn ya hapa jijini Dar es Salaam.

Mimi mwana jf mwenzako ambaye ni mwandishi wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea, ambaye pia ni mtetezi mkubwa wa haki za binaadamu na haki ya kuishi, niko hapa ukumbini kukuletea kile kinachoendelea hapa.

Wakati ukisubiria hii shughuli hapa ianze, karibu nyuzi zangu hizi uanze refreshing

Karibu

Paskali
Naunga mkono hoja ,adhabu ya kifo iondolewe.
Kamwe siungi mkono kabisa kuondolewa kwa adhabu ya kifo hapa Tanzania na hata katika nchi zingine zote kabisa, hususani nchi za Afrika. Sikubaliani kabisa na Hoja hii ya kufuta adhabu ya kifo.
Wapo baadhi ya Wahalifu wanastahili kupewa adhabu ya kifo, na pia wanastahili kunyongwa hadi kufa.
Matahalani, kwa hapa Tanzania kuna Askari Polisi wengi Sana wamekuwa wakifanya vitendo vya uhalifu wa kupora Mali za raia na kisha raia hao wamekuwa wakiuawa makusudi ili kupoteza Ushahidi, watu wengi pia wamekuwa wakiuawa kwa makusudi wakiwa mikononi mwa Askari Polisi au wakiwa kwenye Vituo vya Polisi, na Wauaji wamekuwa hawachukuliwi hatua zozote zile Kali za kuwapa fundisho juu ya uhalifu wao huo. Askari Polisi wamekuwa wakihusika katika uhalifu kama huo kwa kuwa Wana uhakika kuwa na wao hawatauwa badala yake wanahamisika zaidi na zaidi kuendelea kuua watuhumiwa. Mimi binafsi naamini kwa dhati kabisa kwamba Endapo kama Rais wa nchi hii angesaini Hati ya Kifo dhidi ya OCD Christopher Bageni, yule Askari Polisi aliyewaua kikatili wale Wafflanyabiashara wa madini kutoka huko Mahenge Morogoro, Basi Polisi wangeogopa kufanya matukio mengine ya uporaji na mauaji dhidi ya Wananchi.

Aidha, Endapo kama OCD Christopher Bageni angenyongwa hadi kufa Basi lile tukio la mauaji la Bw. Hamza Mohamed pale Selander Bridge Dsm kamwe lisingeweza kutokea, na hata yule Mfanyabiashara kijana wa madini kule Mtwara pia asingeweza kuuawa na wale Askari Polisi walioongozwa na OC-CID Kalanje.

Mwisho:
Namshauri Rais SSH akubali kusaini Hati ya Kifo ili aliyekuwa OCD Christopher Bageni aweze kunyongwa hadi kufa, kwa sababu Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani tayari zimeshatoa idhini na baraka zote kabisa kwamba mtu huyo anastahili kunyongwa hadi kufa. Huku mitaani kuna chuki kubwa sana dhidi ya hao Watu.
Endapo kama Rais anaona labda pengine kutokana na Imani yake ya kidini hawezi kusaini Hati za Kifo ili Watu hao wanyongwe, Basi namshauri AKASIMISHE MADARAKA hayo kwa Watu wengine walio chini yake ili waweze kutekeleza jukumu hilo kwa niaba yake.

Inakera Sana kwa kweli kuendelea kuwaona Watu wauaji ambao waliua wenzao kwa makusudi Halafu wao bado wanaachwa waendelee kufaidi maisha, Kamwe jambo hili halikubaliki hata kidogo.
 
Wanabodi

Tarehe 10 ya October kila mwaka, ni siku ya Kimataifa ya Kupinga Adhabu ya Kifo Duniani.

Kwa Tanzania kwa mwaka huu, Kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu Tanzania, LHRC kinazungumza na Wahariri wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, TEF, katika ukumbi wa hoteli hii ya Holiday Inn ya hapa jijini Dar es Salaam.

Mimi mwana jf mwenzako ambaye ni mwandishi wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea, ambaye pia ni mtetezi mkubwa wa haki za binaadamu na haki ya kuishi, niko hapa ukumbini kukuletea kile kinachoendelea hapa.

Wakati ukisubiria hii shughuli hapa ianze, karibu nyuzi zangu hizi uanze refreshing
Hii event iko live kwenye
View: https://www.youtube.com/live/74qsu__92pM?si=_9Et_u9v2jIC2aN_

Na hapa
View: https://www.youtube.com/live/oJDwqRmsSPE?si=ueIE-gkjwkNpFwPb

Karibu

Paskali

Adhabu ya kifo iendelee kuwepo kwa waliotenda uhalifu unaohusisha uhai wa mwanadamu. Ikithibitika pasi shaka umeua,nawe uuawe,haki mnazoita za binadamu hazikustahili kwani nawe ulikosa ubinadamu wakati ukitekeleza uhalifu. Utapata kinachokustahili juu mbinguni baada ya kunyongwa!
 
Kumetolewa ushuhuda hapa huyu dada mrembo alituhumiwa kuua na kuadhibiwa adhabu ya kifo kwa kunywongwa hadi kufa, huyo dada alikata rufaa, na akashinda na rufaa na kuachiwa huru, akikumbuka aliyokutana nayo, machozi yamemtoka.

P
 
Kuna wengi wamehukumiwa kifo kwa kunyongwa mpaka kufa, lakini hawajakata rufaa kwasababu wala hawajui kuwa wana haki ya kukata rufaa. Hivyo wanasubiri tuu kutekelezwa kwa adhabu hiyo.
Wafungwa wa kunyongwa hawafanyi kazi yoyote, ni kula tuu na kulala, ila wanakuwa na mateso makubwa sana ya kisaikolojia.
P
 
Back
Top Bottom