Swali fikirishi je mamlaka zinazo ruhusiwa kuua?
Hii ni ajabu Sana.
Kumetolewa ushuhuda hapa huyu dada mrembo alituhumiwa kuua na kuadhibiwa adhabu ya kifo kwa kunywongwa hadi kufa, huyo dada alikata rufaa, na akashinda na rufaa na kuachiwa huru, akikumbuka aliyokutana nayo, machozi yamemtoka.
P
Hivyo ni Visa vichache Sana, it is a rare cases.
Naendelea kusisitiza kwamba Kamwe siungi mkono kabisa kuondolewa kwa adhabu ya kifo hapa Tanzania na hata katika nchi zingine zote kabisa, hususani nchi za Afrika. Sikubaliani kabisa na Hoja hii ya kufuta adhabu ya kifo.
Wapo baadhi ya Wahalifu wanastahili kupewa adhabu ya kifo, na pia wanastahili kunyongwa hadi kufa.
Matahalani, kwa hapa Tanzania kuna Askari Polisi wengi Sana wamekuwa wakifanya vitendo vya uhalifu wa kupora Mali za raia na kisha raia hao wamekuwa wakiuawa makusudi ili kupoteza Ushahidi, watu wengi pia wamekuwa wakiuawa kwa makusudi wakiwa mikononi mwa Askari Polisi au wakiwa kwenye Vituo vya Polisi, na Wauaji wamekuwa hawachukuliwi hatua zozote zile Kali za kuwapa fundisho juu ya uhalifu wao huo. Askari Polisi wamekuwa wakihusika katika uhalifu kama huo kwa kuwa Wana uhakika kuwa na wao hawatauwa badala yake wanahamisika zaidi na zaidi kuendelea kuua watuhumiwa. Mimi binafsi naamini kwa dhati kabisa kwamba Endapo kama Rais wa nchi hii angesaini Hati ya Kifo dhidi ya OCD Christopher Bageni, yule Askari Polisi aliyewaua kikatili wale Wafflanyabiashara wa madini kutoka huko Mahenge Morogoro, Basi Polisi wangeogopa kufanya matukio mengine ya uporaji na mauaji dhidi ya Wananchi.
Aidha, Endapo kama OCD Christopher Bageni angenyongwa hadi kufa Basi lile tukio la mauaji la Bw. Hamza Mohamed pale Selander Bridge Dsm kamwe lisingeweza kutokea, na hata yule Mfanyabiashara kijana wa madini kule Mtwara pia asingeweza kuuawa na wale Askari Polisi walioongozwa na OC-CID Kalanje.
Mwisho:
Namshauri Rais SSH akubali kusaini Hati ya Kifo ili aliyekuwa OCD Christopher Bageni aweze kunyongwa hadi kufa, kwa sababu Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani tayari zimeshatoa idhini na baraka zote kabisa kwamba mtu huyo anastahili kunyongwa hadi kufa. Huku mitaani kuna chuki kubwa sana dhidi ya hao Watu.
Endapo kama Rais anaona labda pengine kutokana na Imani yake ya kidini hawezi kusaini Hati za Kifo ili Watu hao wanyongwe, Basi namshauri AKASIMISHE MADARAKA hayo kwa Watu wengine walio chini yake ili waweze kutekeleza jukumu hilo kwa niaba yake.
Inakera Sana kwa kweli kuendelea kuwaona Watu wauaji ambao waliua wenzao kwa makusudi Halafu wao bado wanaachwa waendelee kufaidi maisha, Kamwe jambo hili halikubaliki hata kidogo.