Siku ya kushika mimba ni ipi?

luci

Member
Joined
Feb 15, 2015
Posts
20
Reaction score
6
Habari wana jf. Natamani kuwa na mtoto. Hivyo naomba msaada juu ya siku ya kushika mimba. Mzunguko wangu wa period naanza tarehe 9 na kumaliza tarehe 14.
 
Ninavyoelewa mie, na kutokana na maelezo yako hapo juu, unapaswa ukutane na mwenzi wako kati ya tarehe 1 hadi 8. Ndani ya hizo siku, kiumbe kitapatikana tu
 
Weka wazi nikusaidie. Kuna mizunguko mikuu mitatu. Mrefu siku 31, wa kati(kawaida) siku 28 na mfupi siku 24. Upo wapi?
 
Ninavyoelewa mie, na kutokana na maelezo yako hapo juu, unapaswa ukutane na mwenzi wako kati ya tarehe 1 hadi 8. Ndani ya hizo siku, kiumbe kitapatikana tu

Ahsante
 
Umeolewa? Maana usije kuwa unatafuta mtoto ilhali upo single na yamkini bikra
 
Sawa. Sikia wewe siku ya 15 ndo yai linapevushwa. 15-2=13, 15+2=17. So kuanzia siku ya 13 - 17 ndo siku za wewe kupata mimba. Anza kusex siku ya 12 hadi siku ya 19 kila siku bila kuruka. Mapema sio usiku mwingi. Pia unaposex fanya enjoyeable fikra zenu ziwe ktk kufarahia kusex sio kuwaza mimba. Jiachie ktk kusex. La zaidi muombe MUNGU wako akupe mtoto.
 

Mkuu unamwambia apige game hata akiwa period??
 
Ninavyoelewa mie, na kutokana na maelezo yako hapo juu, unapaswa ukutane na mwenzi wako kati ya tarehe 1 hadi 8. Ndani ya hizo siku, kiumbe kitapatikana tu

ibaraka hapana. Sio siku tarehe hizo. Kama anaanza menses tarehe 9 basi Ovulation itakuwa tarehe tarehe 22, hivyo anapaswa kukutana kati ya tarehe 20 mpaka tarehe 24.
Kwanini? Yai linapevuka siku ya 14 na kwa kuwa linaweza kuwa hai hadi masaa 48(siku 2) na mbegu zinaweza kuwa hai hadi masaa 72(Siku 3)
 
Last edited by a moderator:
uko sawa kabisa
 
aise pole sana ...kama wewe ni mtaalam wa afya utapotosha wengi
 
Last edited by a moderator:

Fuata hicho hapo juu.

Ili kuzielewa kwa urahisi hesabu zako.

Siku ya kwanza kupata hedhi anza kuhesabu, kwa maelezo yako ni tarehe 9. Kwa hiyohesabu siku kumi ambayo itakuwa tarehe 19. Kuanzia tarehe hiyo hadi siku ya 17 tangia siku ya kwanza ya hedhi, yaani tarehe 26, unaweza kabisa kupata ujauzito.

Kwa hiyo zingatia hiyo siku ya 10 toka mwanzo wa hedhi na tarehe ya mwisho 26 kwa kalenda siku zako. Lakini pia unaweza kuanza kukutana kimwili na mwenzi siku ya 7 na kwa kalenda yako itakuwa tarehe 15, hii ni kwa kuwa mbegu za kiume zinaweza kukaa hai kwa siku 3 zikusubiri kurutubisha yai la kike.
 
Habari wana jf. Natamani kuwa na mtoto. Hivyo naomba msaada juu ya siku ya kushika mimba. Mzunguko wangu wa period naanza tarehe 9 na kumaliza tarehe 14.

Pole sana ndugu yangu maana unaonekana hauna elimu ya siku zako,ngoja nikufungue macho.
Haiwezekani mizunguko yako kuanza tar9 na kuisha tar14 coz mwisho wa mzunguko mmoja ni mwanzo wa mzunguko mwingne,kwa hiyo achana na tarehe zitakuchanganya.Kwa nilivyokuelewa ni kwamba mzunguko wako unasiku 35,hii ni moja kati ya mizunguko mrefu.
Ngoja nikueleze kirahisi sana
-Pindi unapoona damu zinatoka(hedhi) ujue ni siku yako ya kwanza ya mzunguko
-Endelea kuhesabu siku kwa mzunguko wako wewe siku za kupata mimba ni siku ya 18 hadi ya 24 toka hedhi ilipoanza,kwa hiyo siku hizi zitumie vizuri saana.
ZAIDI YA HAYO
-Siku ya 21 yai la kike huwa linatoka kwenye ovari kwa mzunguko wako.
-Siku ya 18 hadi 20 ni siku ambazo kuna uwezekano mkubwa wa kupatikana mtoto wa kike
-Siku ya 21 hadi 22 mtoto wa kiume
-Siku ya 23 hadi 24 hazna uhakika sana
 
Nina mzunguko wa siku 31

Siku za Kupata Mimba Ni Siku ya 15 kutoka Siku ya 31... yaani 31,30 29 28 27 26 25 24 23 22 21 20 19 18 17 na 16 .... hiyo siku ndipo Yai linakuwa Lipo tayari na Homoni zako za Uzazi zipo juu hasa LH.... Kwahiyo Ukifanya tendo siku hiyo utapata Mimba..

Kwahiyo Kama umebleed kuanzia tarehe 9 na umemaliza leo tarehe 14 kwahiyo siku ya Yai kutoka Itakuwa Tarehe 23/3/2015 au 24/3/2015 kwahiyo ni Vyema Ukasex Siku hzo au Siku moja Kabla Ya Hizo na Ukaendelea Mpaka 26...

WARNING: Hakikisha Style unayofanya Isiwe ya Kutoa Mbegu nje ya Uke wako... Au kuzifanya zimwagike





Pia Zipo Dalili za Nje Ambazo unaweza Ukawa Unazihisi

1. Kupanda kwa Joto la Mwili mpaka 40

2. Kuwa na Hamu ya Tendo la Ndoa na Kuwa na hamu ya Kuwa na Mwanaume kwa Sex

3. Uke kuwa mlaini na ute ute tofauti na siku nyingine

Mtoto wa Kutegemewa sana Skku hiyo ni wa Kiume .. GOOD LUCK
 
Uko sahihi kabisa, ulichoeleza ni kuhusu siku ktk mzunguko, yaani akiona damu leo, hiyo ndo cku yake ya kwanza kwa hiyo aesabu mpaka 13 hadi 19 ndo cku nzuri za kumimbishwa. pia asitumie tarehe za kwenye kalenda bali ahesabu cku ktk mtindo huu.
 
Ikiwa mtu ana mzunguko wa cku 22 cku za hatari ni zipi na safe ni zipi? Msaada hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…