Siku ya kutahiriwa

Bado anagovi anataka apate xperience kwanza, ajiandae kisaikolojia

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa taarifa tu, tungekuwa tunatahiriwa kwa mara ya pili(kwa ambao tuliotahiriwa tukiwa wakubwa, nilitahiriwa nikiwa na miaka 14) ningempiga mtu na mshale akitaka kunitahiri. Haya maneno aliwahi kuyasema Mzee mmoja kipindi nauguza kidonga cha kutahiriwa.

Kutahiriwa sio ishu, ishu ni kuuguza kidonda
 
Mie nilitairiwa nikiwa std 1au 2, siku hyo tulikuwa mm na bro tunaefuatana kuzaliwa. Kabla yetu aliingia jamaa mmoja nadhani alikuwa kwny 20s, jamaa alikuwa analia kama ananyongwa vile, mzee akatuuliza vp tukasema tuahirishe, akagoma.

Bro akaingia kabla yangu, by the time namaliza namkuta jamaa anajiviringisha kwny sakafu, kisa ganzi imeanza kuisha, na mie yakanikumba baada ya kama 30 mins. Ni experience moja mbaya sana, especially ukishuhudia mtu mwingine akifanyiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka Mzee alituvalisha nguo MPYA akasema twendeni safari nilikua na bro daah nikakuta tunashuka hospital Mara pap "washike wasikimbie" Mara paa "leteni mikasi " Mara paap "wavalishe kanga

Tukarudi home walemavu Wa mwendo
 
Mkuu umenikumbusha mbali sana, binafsi nilifanyiwa hiyo kitu nikiwa mdogo sana hata chekechea sijaanza, sasa baada ya shughuli na kidonda bado kibichi na mimi mbishi naenda kucheza kama kawa, kila mama akinirudisha nyumbani mm natoroka kwenda kucheza.

Sasa siku ya siku siafu wakaingia ndani ya bandeji mm sina habari wakahisi kubanwa ikabidi na wenyewe waanze kushambulia........mpaka leo nakumbuka kilichonipata maana toka siku hiyo sikutoka nyumbani tena mpaka nilipotolewa nyuzi!!!!
 
Mkuu, huko wanaume kama mimi si wanaweza wakanichoma moto kwa hasira...!!??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka Mzee alituvalisha nguo MPYA akasema twendeni safari nilikua na bro daah nikakuta tunashuka hospital Mara pap "washike wasikimbie" Mara paa "leteni mikasi " Mara paap "wavalishe kanga

Tukarudi home walemavu Wa mwendo
We jamaa stori yako inachekesha sana kama komedi vile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…