Siku ya kwanza kijiweni kama dereva bodaboda

Hao ndo wale ma last born wachagua kazi
 
Kama upo kigamboni uwe unawahi pale uhasibu kuanzia saa 10 alfajiri pale pesa hatari ,mida hiyo hakuna kabisa bodaboda

Pili na muhimu Sana ,vaa helmet muda wote na usiwe na haraka barabani na jitahidi Sana ufwate sheria

Kingine Kama pikipiki Ni mpya uwe makini kupakia abria wa kuingia vichochoroni
 
Hongera, itapata pia mademu wa kugonga...
 
Mkuu nimeku PM
 
Yaah nipo Dar mkuu Kigamboni
Nakushauri ukiweza unaweza ku-park kariakoo

Kama una ndugu au jamaa yako (mwenye biashara kkoo) anaweza kukudhamini madukani ongea nae halafu mpite madukani akutambulishe ukipatikana mzigo unapigiwa simu unawapelekea wateja

Ukifanya mizigo inaweza kukulipa zaidi
Mf:kutoka kkoo kupeleka mzigo fire 5,000
Mbezi stendi ni 12,000
Kwa siku ukipata mizigo hata 6 inatosha



Ni uaminifu tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…