Siku ya kwanza kuingia boarding school ya government

Siku ya kwanza kuingia boarding school ya government

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Ilikuwa form V, baada ya orientation, tunes za kujuana. Wengi tulishapewa majina ya rafiki wa rafiki ambae anakuja shule ile.

Dining siku ya kwanza mdada mmoja akimwaga magarage kisa alimkuta mende ndani ya bakuli. Kwakuwa bado tulikuwa na makula kula kuna waliomtengenezea orange squash na marie biscuits.

Baada ya miezi miwili pale shule, mdada alikuwa hodari wa kutoa mende kwa kijiko na kuendelea na menu.
 
Hahahahahaha tulipewa zoezi la kuimba wimbo mmoja eti "Rungu la mchawi wiwi wiwi wiwi wiwiwi wiwi wiiiiiiiiiiiiiiiii!!!!" huku tunatembea kwa kasi na hatua kubwa kubwa katika eneo ambalo tukipiga hatua nyingi basi ni tatu tu na tunatakiwa kutoka point A tukifika point B tuwe tumeshamaliza kuimba...Ukifeli ni kichapo kikali sana, na hakuna aliyewahi kufaulu na haitokaa itokee. Tulikuwa tunaishia... "Rungu la mcha.." tayari tumefika mwisho
 
kumpeleka mtoto shule za boarding ndio nafasi kwake kwenda kujifundisha uhuni
 
Enzi zile kwenye mchaka mchaka mchaka tulikuwa tunaimba “Kambona ameolewa huko Ulaya. Tuliaminishwa kuwa ni mhaini kumbe alikuwa mpinzani.
 
Mimi nakumbuka nilienda ni kibakuli changu cha kupasuka kwaajili ya mboga na uji lakini baada ya mwezi nilianza kutumia kile kisadolini cha sabuni ya unga cha lita tano kwaajili ya mahitaji madogo madogo ya tumbo
 
Back
Top Bottom