siku ya kwanza kula kwa kisu na uma

apprentice1997

Senior Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
107
Reaction score
99
Tukumbushane Mara ya kwanza kura kwa kisu na uma ilikuwaje, Mimi nilibahatika kushiriki conference nyingi kubwa Mara zote nikawa nakula kisu naweka kushoto uma kulia basi nikazoeahvyo mwaka huu nikala na rafiki zangu wazungu walipoona nimefanya hivyo wakanambia nisipate shida kula vile nadhani walijikaza wasicheke ila baadae nikaalikwa kwenda kwenye dinner ya maana . mlimani city nikagoogle nakuja shtukia kumbe una unakaa kushoto kisu kulia nilicheka sana ushamba umezidi japokuwa bado sijawa pro bado najifunza
 
Kutumia hivyo vitu mimi nishashindwa ,yaani nakula kuku au samaki halafu nitumie uma ,? Wacha niwe mshamba tu nitakula na mikono yangu
 
Bora nyie mmeshindwa hivyo mimi baada ya kupata kazi ya kwanza ya kampuni yetu mi na mwenzagu tulialikwa Na MD wa kampuni hiyo iliyotupa kazi SA, jamaa akatualija dinner bana katika kuagiza si nikaagiza cosmopolitan cocktail, jamaa yangu nae akaagiza hiyo hiyo aisee, ilivyokuja tuu niliona noma sana kwanza yule mwenyeji wetu aliuliza kama huwa tunatumia hiyo tukamwambia hicho ndo kinywaji chetu tunachopenda ha ha ha

Mwenyeji wetu ye kaagiza beer
 
mimi ukweli niseme ushamba wangu...kuna siku nikuwa hapa kuleana mwanza nikaagiza chapati chai na matunda, wakaniletea na kisu na ummaa bila maji ya kunawa,xo nikajifikilia sana nileje au niende kunawa, nikapiga jicho pembeni nikaona tissue za kujifuta maji.nikaamua kuchukuwa moja taratibu nikaendelea, cha ajabu akaja mteja mwigine akaagiza chapati.wakaleta vile vitu tena nikamcheki kwa makini bila yeye kujua.nikaona anakatakata kwa ustadi sana chapati kisha akachukuwa UMMA na kuanza kula, nilikifunza kitu toka hapo..
 
Mara nyingi ushikaji wa kisu au uma unategemea na wewe huwa unatumia mkono gani.. au mkono gani una nguvu zaidi.. either mashoto au malia..

Ila pia Unaruhusiwa kubadilisha mikono.. inategemea unakula nini..
 
hayo mambo sisi waafrika hayatusaidii lolote,kifupi ni utumwa tu huo,jiongeze na ujitathmini jinsi unavyosikitisha kwa huu uzi ulouleta
 
Kisa changu mimi ni tofauti kidogo, tulikwenda camping na wadada wa kizungu, usiku tulikuwa na sandwich tulizobeba na matunda tulikula na kulala kwenye mahema. Asubuhi tuliwasha jiko la gas, nataka kupasha moto baked beans kwaajili ya breakfast, ndiyo tunagundua hakuna tin opener, niliwaauliza kuna kusu? Walinipa kisu cha jikoni nikafungu kopo, wale wadada wote walitoa macho, niliwajibu kwetu jikoni hiki kinamaliza shughuli zote, baada ya kuchinjia kuku, damu inasafishwa kinakata nyanya na kitunguu.
Ninadhani walienda kusimulia makwao, mtu anaeweza kufungua kopo kwa kisu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…