Acha tu mkuu usiombe awe hajafunga macho
Je, uliisikia ile ya Musoma? Boti ilipinduka watu wakazama, wakaokotwa wachache tu. Siku ya siku mvuvi si akavua Sato mkubwa? Alipomchinja akakuta mkono wenye saa tumboni. Hii ilivuma sana tuAisee kama Movie vile duuh inatisha sana hii
Pole sana mkuu, upande wangu ni tofauti sana nimeona maiti mara ya kwanza kwenye ajali ya gari nikiwa darasa la tano na nyingine kuna jamaa aliuwawa na tembo lakini niliona easy tu kwa kweli mpaka leo hata ikitokea msiba wananiambia nikakague maiti.Hakika kila nafsi itaonja mauti japo kifo hakizoeleki kabisa ndo maana huwa tunaumia sana tukifiwa.
Kuna siku niliona maiti ya mmama aliegongwa na gari nikiwa la saba aisee ile picha haijawahi potea kichwani mwangu ubaya alikuwa bado amefungua macho[emoji24][emoji24][emoji24] Baada ya lile tukio alifariki rafiki yangu hakika sikuweza kwenda kuaga nilishindwa kabisa! Mungu awalaze mahali pema peponi.
Je siku ya kwanza kuona maiti ilikuwaje?? Hii memory ni mimi tu nashindwa kuifuta au?
Duuh una moyo mkuu...Tembo ana hatari aiseePole sana mkuu, upande wangu ni tofauti sana nimeona maiti mara ya kwanza kwenye ajali ya gari nikiwa darasa la tano na nyingine kuna jamaa aliuwawa na tembo lakini niliona easy tu kwa kweli mpaka leo hata ikitokea msiba wananiambia nikakague maiti.