Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
" Yep! Yap! Yep! Yap!
Swapswapswap!
Yep!yep! Yap! Yep! Yep! Yep!yep!
Kiuno! Up! Dancedancedance!
Magoti Tap! Jumpjumpjump!
Bend down! Downdowndown!"
Mwalimu anarudiarudia kuimba kipande hicho akisaidiwa na mdundo WA muziki mkubwa, kifuani kwake kulichomekwa maiki ili Sauti yake isimezwe na mdundo, huku tukiwa tumepanga msururu Mbele ya Kioo kikubwa kilichoonyeshwa taswira zetu zikiwa Zimesenuka, zimechemka miili ikiwa inatoa jasho.
Tulikuwa watano, mwalimu akiwa katikati yetu akitutenganisha wanafunzi wawili huku na wengine wawili huku. Hivyo walikuwepo wanawake watatu, na sisi wanaume wawili.
Tuliendelea na zoezi huku muziki ukibadilika badilika na kuchochea hamasa za kila mmoja wetu. Labda ulifikiri Mimi ni mzoefu, nooo! Sikuwa na uzoefu wowote. Hii ilikuwa siku yangu ya kwanza kufika Gym. Lakini nilijifanya kama mzoefu wa mambo ya Gym ili nisionekane mshamba.
Nilikuwa nimevaa raba Kali ya mazoezi, na bukta ya mazoezi ndani nikiwa nimevaa taiti zile zakiume za mazoezi juu nilikuwa nimevaa zile flana zilizoacha makwapa wazi. Unafikiri nilisahau kuweka wireless Earphone moja sikioni, thubutu! Ningeachaje, ili nionekane wakuja.
Nilipiga hiyo earphone, halafu mkononi nikawa nimefunga sijui ni bandeji sijui wanaitaje Ile plasta, basi ilimradi nami nionekane.
Kichwani nilivaa Rubber ungedhani mtoto wale wachezaji wa Cricket, yaani ungeniona ungejua Mimi ndio Gym Trainer, kumbe...!
Baada ya kukaribishwa, ilinibidi nibadilishe mwendo Kwa muda ili niendane na pigo za Gym, unavuta pumzi ndani kidogo, kifua kinajaa, unatanua kifua na mikono kidogo kisha unatembea ukiwa unadunda katikati ya mwanamuziki na mwanamazoezi, hayo ni mambo ya Gym hayo. Basi sikutaka kusahau kutafuta bite na hapa nazungumzia BIG G ili nitafune ati ili kujipa umakini. Si unajua ukitafuna Akili inatulia. Ndio mambo hayo.
Sikusahau kuchukua chupa ya maji niliyoiweka kwenye kibegi changu, nikaitoa kwenye begi na kufungua kifuniko alafu nikanywa kama fumba mbili hivi nikiwa najitazama kwenye Kioo kikubwa ambacho pia kiliwaonyesha Watu wengine niliowakuta.
Sikuwa na muda wa kuwaangalia ili kujifanya mimi ni mwenyeji wa mazingira kama yale. Labda niliyaona mazingira yale kama yakawaida, lakini kiukweli hayakuwa yakawaida.
Ilikuwa gym ya kisasa kabisa iliyokuwa juu kabisa ya ghorofa, upande wa Kusini na Magharibu kwa chini ilikuwepo bahari na mandhari ya kuvutia. Ni huko Mikocheni.
Vifaa vya mule ndani vilikuwa vya kiteknolojia vizuri na vyakisasa, kiyoyozi kikipenya vyema katika mapafu yangu.
Baada ya kunywa maji, macho yangu yalipokelewa na wanawake wawili, wakiwa kwenye vifaa vya mazoezi wakiwa wanakimbia juu ya vifaa vile vilivyokuwa vinateleza hali iliyowafanya warembo wale wasiende mbele wala nyuma licha ya kuwa walikuwa wakikimbia. Hilo halikunishangaza, wala isingekuwa habari kwangu.
Kilichonikausha maji ya mwili ni jinsi walivyo, walikuwa wanawake wenye miili ya ajabu yenye kusisimua, nilitaka kuwa I don't care, lakini macho yangu yalishuka chini ya kiuno ambapo nilipokelewa na mneso wa ajabu.
Yalikuwa yakinesa nesa, mithili ya nini sijui, nikasema I don't know, kumbe sijui yalikuwa yananisikia niliposema hivyo nikashangaa yakaanza kunesa nesa zaidi, kadiri walivyozidisha Kasi ya Mashine na wao kukimbia, ndivyo mineso ikazidi kutikisa wezere. mineso ikanipa mateso, nikawa nimebaki nimesimama nimeshika chupa la maji.
Vile visuruali vyao walivyokuwa wamevivaa ndio viliua kipa na beki wangu. Sasa ni wao kupiga tuu shuti Mpira uingie wavuni.
Mara Gym Trainer akaniita, huyu ndiye aliyenipokea kule mapokezi, huyu ndio alikuwa kiboko, unajua kule mapokezi sikuwa nimemuona vizuri kwani alikuwa kwenye kichumba cha ndani, hivyo nilimuona kuanzia kifuani mpaka kichwani.
Nilitaka kujisalimisha Mbele yake, alikuwa Mwanamke mwenye Rasta, Mjamaica, mwenye rangi ya Kahawia, macho makubwa na midomo mine ungedhani ni zile katuni za magazeti, shepu yake ilinifanya nihisi aliyembele yangu ni Jinni chotara mwenye mchanganyiko wa Jinni na Malaika.
Yeye hakujali kubabaika kwangu, bila shaka alijijua yeye ni mzuri sana, niliwahi kusimuliwa hadithi ya Majini yaliyochumbia Malaika walioasi. Hakuwa mbali na viumbe hao.
Nikakumbuka kuwa ninapaswa nisijisahau kuwa mimi ni mzoefu. Yule Dada akaniambia ninatakiwa nifanye mazoezi ya yoga kwanza, tukaenda kwenye yoga, Huko akawa ananielekeza, mimi hata sikuwa na akili.
Mapigo yangu ya moyo yalikuwa hewani ungedhani mtandao wa starlink. Hisia zangu zilipeperushwa mbali katika anga lenye tufani za mapenzi, mbaya zaidi anga hilo lilimilikiwa na hili toto zuri ambalo muda mwingi macho yake yalikuwa yananiangalia ungedhani ananitamani kumbe ndivyo macho yake yalivyo, yalikuwa macho makubwa mlege.
Unajua hawa Jamaican women wanapenda sana muziki, ni kama walilogwa nao. Kwa waliowahi kuishi na wanawake wakijamaica mtakubaliana nami kuwa hawa ndugu zetu wanapenda sana muziki na michezo ya yoga, martial arts kuliko kula.
Hivyo huyu mrembo ndiye gym Trainer wangu alikuwa akicheza huku akikata mauno na kuninengulia, sijui alikuwa anataka nini.
Mimi nikanichanganya, nikadhani ananitaka, nikambambia Mimi, nimechoka na mineso, Oyaa! Wanangu sio poah! Kama sio kujua michezo ya ngumi ningekutana na kitu kizito. Gym Trainer akarusha Jab nikai-block, akawa kama anataka akarusha Winchu! Nikaikwepa ikakata upepo, nikamdaka nikamtuliza.
Baada ya hasira zake zikaisha, akanisifu Kwa namna nilivyojua kupangua mapigo yake. Huku akitaka kujua nina ujuzi wa mapigano. Nikamuambia Mimi ni street fighter tuu, nilibahatisha. Gym Trainer akaanza urafiki na Mimi tukabadilishana mawasiliano.
Siku Ile ikapita kama ilivyo, nikawa naenda mara mbili kwa wiki. Kumbe bana mwanamke mzuri sio mmoja. Juzi hapa ilikuwa sio pouwa! Hilo chuma nilichokikuta huko Gym sijui kama nitapona. Nahisi mimi sikuandikiwa kwenda peponi, sio kwa kazi ile niliyoiona. Kazi zile kuzifukuzia ni lazima uuze roho,
Subiri! Ngoja nimeze mate.
Sikuchelewa, mimi na pisikali! Thubutu! Anaitwa Santa! Ndilo jina lake. Hapo ndipo yataka moyo, mambo kama haya kwenda jehanamu ni uhakika lakini nani atajali. Mimi? Au wewe? Au yeye? Mimi nikivurugwa navurugwa Kweli.
Naendelea ngoja ninywe maji....
Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Gym, Dar es salaam.