Siku ya kwanza napanda lori nilikuwa natoka Mwanjelwa Mbeya naelekea Dar es Salaam. Niliomba njia nzima, nikashuka Morogoro, chakufia nini?

Nilipanda Howo,ilikua ina tela la kontena lakini halina kontena,kila shimo tela likipita huku mbele wote mnacheza,ilikuwa ni mwendo wa kurukaruka,zile km takribani 30 zilikuwa ngumu sana kwakweli...
 
Nilipanda Howo,ilikua ina tela la kontena lakini halina kontena,kila shimo tela likipita huku mbele wote mnacheza,ilikuwa ni mwendo wa kurukaruka,zile km takribani 30 zilikuwa ngumu sana kwakweli...

Usafiri wa Malori lazima úwe na kipaji.
Alafu kuna Watu hizô ndîo safari zào. Yaani kupanda Basi au Ndege Wanaona shida
 
Pole sana ila usafiri wa lori ni mzuri mara nyingine una changamoto sana.

Mengi yanatokea, kuna siku napanda makambako pale dereva alimuacha konda wake kama utani. Haya mabishano mabishano tu. Dereva akawasha chuma na kusepa.

Uzuri wa tank ni mwendo wa basi tu ukiwa unaenda dar maana zinakuwa tupu.

Haya machuma mengine muda wowote ule unalala njiani. Jamaa huwa hawana haraka. Dar moro mnaweza kulala.
 

Mkûu sikujua kama Malori ya Mafuta yanatembea kiasi Kile.

Utaniutani wanakasirikiana kwelikweli
 
Maisha yaache yalivyo.
Yakiamua kukufundisha hata usipotaka utafunzwa tu.
Pole sana Mkuu
 
Sijui kama ungekuwa mtwara huku njia ya kusini ungependa malori maana dangote kila siku lazima aangushe gari...me huwa napanda sana special haulers za makaa ya mawe
 
Nimecheka sana, sasa ungepanda pikipiki BMW 1200/1250/1600na ukamkuta rider mwenye kifua, si ungejinyea?
 
Hizo safari kama safari ya kuzimu.

Kûna Moja nilikuwa natoka Vatican maeneo ya Kibati, Turiani Morogoro. Usiku kucha tukiwa tumebeba MAITI. Noma Sana
Kuna moja mimi ndiyo niliiona ya Kingese sana. Mida saa 4 usiku, usafiri bilabila, na utamaduni wangu nikishaaga sirudi wala silali nipo tayari nitembee kwa mguu angalau kilimeta 25 nikapale mji unaofuata lakini si kubaki sababu eti nimekosa usafiri.

Imefika saa 4 usiku Scania hiyo imesimama, pale iliposimama kulikuwa na abiria kadhaa ambao walishaanza kukata tamaa na wengine kwenda kutafuta vyumba karibu.

Mimi nikawa nimejipa dakika 40 za kusubiri kabla sijaanza kutembea kwa miguu ili kusogea mdogomdogo.

Iliposimama tu, abiria tukawa watatu, mimi, jamaa fulani tuliyekuja kujus kuwa ni mwalimu, na dada mmoja mweupe mwenye muonekano wa Kinyarwanda halafu usafiri mbovu (yaani matege ya nyuma na ndani, ila yanamfanya avutie kichizi). Huyo Mwalimu muda huo tayari alikuwa na wenzake wengi sana kichwani (yaani alikuwa amelewa sana)

Tukapanda Scania, safari ikaanza huku yule mwakimu na wenzake alii nao kichwani wakitupigia makelele, uzuri hakuwa anaenda mbali maana aendapo ilikuwa ni kama Km 18 kutoka tulipopandia, lakini akashindwa kupatambua anaposhukia. Nikamstua dereva kwamba sipajui anapoenda yule jamaa ila kwa pale tulipofika nina uhakika tumeshapatita kwa km 15 zaidi.

Yule jamaa anazidi kupoteza network ikabidi nimeambie dereva asimame kijiji hicho tulipo, nikashuka na yule Sokomoko,(Mlevi), dereva akataka tumshushe kisha tusepe nikasema hapana, maada tumejua ni Mwalimu, ngoja nimkabidhi kwa watu, maana lolote linaweza kumpata usiku huo halafu nikajikuta nabaki na hatia wakati nilikuwa kwenye nafasi ya kuweza kufanya jambo kuzuia maafa.

Muda huo vijijini watu wameshalala, nikaona kwa mbali kama kuna kiduka au kijiwe sugu kina wazee wa wawili na bodaboda mmoja wanasogoa, nikawasalimia , nikawaelezea na kumkabidhi yule, wale Wajamaa wakanishukuru nikawashukuru nikarudi kuendelea na safari.

Kama ujuavyo, automatiki jamaa ndiye akawa story mule kwenye gari. Huku dereva na yule dada wakinishangaa sana pia kunipongeza kwamba ni kati ya binaadam wachache (hilo hata mimi nalijua, kama hutaki unaacha).

Basi ikawa wakinipakulia minyama mimi nikawa naziua, yule dada nikaona analeta ucheshi ila bahati mbaya I'm not good at ucheshi, nje ya hizi simu na vi emoj ni heri ukaishi na dubu au nyati au hata mamba kwenye maji wanawaeza wakakupa smiling faces lakini siyo mimi.

Kwenye cabin ya ile gari kuna jamaa alikuwa amelala, ni mwenzake na dereva. Safari ikaendelea demu alipoona sina story akageukia kwa dereva, wakapigapiga story mara akataka kumfahamu yule mwenzake na dereva maana alikuwa ameshaamka.

Story za hapa na pale, lisaa limoja lililofuata wakawa wanaongea wenyewe, dem akadai amechoka anahisi kusinzia, jamaa akamwita kwenye cabin, dem akahamia nyuma.

Wakati dem anahamia kwenye cabin nyuma akaniomba nimuwekee simu yake pale nilipokaa, muda wote tangu tukiwa pale chini nilisahau au sikuzingatia kumuangalia chini ya kiuno upande wa mgongoni. Wakati huu anahamia nyuma ndiyo kwa bahati mbaya nikajikuta nimemuangalia maeneo ya nyuma, aisee, palikuwa pamevimba vizuri halafu laini mithili ya nundu ya ng'ombe wa kienyeji, yeah, ni lazima nisifie, nina moyo hai mimi siyo toy. Ni vile sema sisi wengine siyo mafundi Beatle.

Tangu bint amehamia nyuma dakika 5 mbele nikaanza kusikia watu wananong'ona, dakika mbili zilizofuata nikasikia purukushani za watu wakigeuzana sijui, mara nikasikia kama nguo zinalazimishwa kutoka mwilini, nilipoanza kusikia miguno nikakumbuka nina earphones. Kuanzia hapo sikuhusika na yaliyoendelea (ila nina uhakika pale lazima lilifanyika kosa kama la marehemu) isipokuwa simu ya yule dada ilikuwa ikiita mara kwa mara na mpigaji alikuwa ameseviwa kama "Don Dodoma".

Walipomaliza kutenda Sambi Syao , yule dada akarudi kukaa mbele na kutaka kujichangamsha (Kumbafu zake, atiwe huko halafu anisemeshe-semeshe mimi?). Baadaye "Don Dodoma" akapiga simu, yule dada akapokea, jamaa akauliza vipi mbona nimepiga simu muda mrefu haupokea, dem akajibu kuwa alikuwa amelala ila baada ya masaa matatu atakuwa ameshafika. Kumbuka tulitoka saa 4 usiku, na muda huo ni kama saa saa 7 hivi usiku. Jama akamtakia dem safari njema (asijue muda wote alipokuwa akipiga simu lakini haipokelewi, demu alikuwa yupo kuliwa kimasikhara).

Usiku kwa usiku, safari ikaendelea, gari ikafika mkoa ambao mimi nashuka na dem kumbe anashuka pale gari inabidi ielekee mkoa mwingine na mimi naelekea mkoa mwingine ila dem akawa ameshafika, hiyo tayari ni saa 9 inaenda 10 ya Manane. Namuangalia demu anahangaika kufungua pochi yake, akavuta vazi jeusi akajitanda mwilini, kichwani akajifunika ile kizanzibari tayari amekamilika, mimi namalizia kushusha begi langu la mgongoni simu ya dem ikaanza kuita tena na mpigaji ni yuleyule Don Dodoma.

This time dem hakupokea akasikea na kusimama kwenye barabara ya waenda kwa miguu, pembeni ikasogea gari, akashuka jamaa (Don -Dodoma) . Yes ndiye huyu hakulala usiku mzima akimsubiri mpenzi wake na sasa amekuja kumpokea.

Nikadhani ile ilikuwa ni bahati mbaya tu, safari 3 zilizofuata kwa mtiririko usiofuatana nikashuhdia hayahaya, wakati mwingine mnajikuta mnalinda gari huku dereva na abiria mwenzenu wameenda kufanya matusi...kwa kifupi ni Usafiri Kafiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…