Siku ya kwanza niliponunua gari

illegal migrant

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2013
Posts
1,277
Reaction score
1,121
hii siku sitaisahau kwani ilijaa vituko vya kila aina, kwanza nilikuwa nafanya mizunguko isiyo ya lazima si unajua tena kipya kinyemi du nikamaliza akiba yangu yote kwa kuweka mafuta nilizunguka jiji lote mara kigamboni mara bagamoyo ilimradi tu nione raha, nikaingia kwenye foleni daladala ikanikwangua bila kujua kama mimi ndo mwenye makosa kwani nilikuwa naingia barabara kuu, nikakomaa mpaka polisi akaja

Baada ya polisi kuja akanisambulia kwa maneno kisha akaniambia "ndo maana unaendesha gari la kike" nikatoka nikarudi zangu hom du nikaanza kuliosha gari yaani sikuwa na muda hata na shemeji/wifi yenu nikashinda kwenye gari huku nikibadisha mziki kwenye mp3 nikamuomba shemeji yenu aniletee chakula kwenye Gari nikala ikawa ni usiku tayari nikaendelea kusikiliza muziki mpaka nikasinzia akaja shemeji/wifi yenu kuniamsha "mume wangu twende ukalale ndani hapo kuna mbu" nikamjibu kwa ukali achana na mimi basi akanishauri aje na net aifunge kwenye gari nikamzaba kibao

Nikajikuta umeshakuwa asubuhi na na ule mziki hauimbi tena kumbe betri ilikuwa imeshanyonywa nikajaribu kuwasha gari likagoma kuwaka nikarudi kwa mwarabu aliyeniuzia gari nikamshambulia kwa maneno nikimshutumu kuwa ameniuzia gari bovu akanielewesha kuwa mziki niliosikiliza usiku kucha ndio umenyonya betri akanisaidia gari likawaka nikaondoka kuelekea nyumbani,

Njiani nikasimamishwa na askari nilikuwa sina cha kuzimia moto akanipiga faini elfu thelathini akamaliza akiba yangu yooote nikarudi nyumbani mpole waifu akaniambia aise hili gari naona limeleta balaa...wewe ilikuwaje?
 
Hahahahaa,mdau umenichekesha sana asbui hii,nashukuru kupitia uzi huu ntapunguza baadh ya changamoto NIKINUNUA USED CAR
 
haha duh!! hii kali inaonekana ulitaka ukifa uzikwe nalo kabisa hahaha
 
Ngoja siku nikinunua nitaandika hapa
 
mbona hujasema kupiga honi mara kwa mara! bila shaka na huo mziki wako ulikuwa unafungulia sauti ya juu...kweli maskini akipata m.at.ak.o hulia mbwata!
 
duuh ndio changamoto hizo mkuu, na kufunga funga breki najua kulikuwepo tu
 
Mimi siku ya kwanza nalitoa bandarini nilimgonga mtu nikaishia Central.Kiukweli nilikuwa embarrassed sana. Baada ya hapo nilimaliza wiki nzima sijaligusa.
 
Hahahaa, mimi ngoja nivute kumbukumbu siku nimenunua baisikeli yangu foneksi ilikuwaje kule kijijini!
 
Aisee nimecheka sana. Mengine yananihusu hatamimi. Hasa hilo la kuzunguka zunguka na gari bila issue yoyote. kwa sasa naendesha kwa mwezi mara nne yaani kila jumapili tu kwenda kanisani.maana niligundua nilinunua gari huku akati sina uwezo wa kulifinance(kuligharamia).niligundua pia nikiwasha gari moshi unaotoka unaashiria hela imeanza kuungua tayari
 
Bila kusahau kumsalimia kila mtu unayemfahamu kwa sauti ya juu hata kama yupo karibu ili akuone na kulifuta futa vumbi kila saa.
 
Yaani nipo humu chumbani nacheka km mwehu kwa uzi wako huu,nashukuru cko kwn daladala,ubarikiwe kwa kuing'arisha cku yangu
 
Mbona hujasema kusimama na kusalimia kila mtu unayemfahamu au kuwapungia mkono ili wakuone.
 
Me Siku yakwanza niliipark kwa jirani ili tu ka bint kake kajue na mkoko nakweli nilikamega mno.do its golden old days kwakweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…