illegal migrant
JF-Expert Member
- Oct 18, 2013
- 1,277
- 1,121
hii siku sitaisahau kwani ilijaa vituko vya kila aina, kwanza nilikuwa nafanya mizunguko isiyo ya lazima si unajua tena kipya kinyemi du nikamaliza akiba yangu yote kwa kuweka mafuta nilizunguka jiji lote mara kigamboni mara bagamoyo ilimradi tu nione raha, nikaingia kwenye foleni daladala ikanikwangua bila kujua kama mimi ndo mwenye makosa kwani nilikuwa naingia barabara kuu, nikakomaa mpaka polisi akaja
Baada ya polisi kuja akanisambulia kwa maneno kisha akaniambia "ndo maana unaendesha gari la kike" nikatoka nikarudi zangu hom du nikaanza kuliosha gari yaani sikuwa na muda hata na shemeji/wifi yenu nikashinda kwenye gari huku nikibadisha mziki kwenye mp3 nikamuomba shemeji yenu aniletee chakula kwenye Gari nikala ikawa ni usiku tayari nikaendelea kusikiliza muziki mpaka nikasinzia akaja shemeji/wifi yenu kuniamsha "mume wangu twende ukalale ndani hapo kuna mbu" nikamjibu kwa ukali achana na mimi basi akanishauri aje na net aifunge kwenye gari nikamzaba kibao
Nikajikuta umeshakuwa asubuhi na na ule mziki hauimbi tena kumbe betri ilikuwa imeshanyonywa nikajaribu kuwasha gari likagoma kuwaka nikarudi kwa mwarabu aliyeniuzia gari nikamshambulia kwa maneno nikimshutumu kuwa ameniuzia gari bovu akanielewesha kuwa mziki niliosikiliza usiku kucha ndio umenyonya betri akanisaidia gari likawaka nikaondoka kuelekea nyumbani,
Njiani nikasimamishwa na askari nilikuwa sina cha kuzimia moto akanipiga faini elfu thelathini akamaliza akiba yangu yooote nikarudi nyumbani mpole waifu akaniambia aise hili gari naona limeleta balaa...wewe ilikuwaje?