Siku ya leo Nimetimiza miaka 37 lakini mambo bado

Happy birthday!! Tuko pamoja mkuu. Jana nimegonga 51 lakini assets zangu ni vyeti na vitabu tu. Kinachoniliwaza ni kuwa nikifa sihitaji kujizika. Kutakuwa na watu wa kunizika. Wasipokuwepo, halmashauri ipo. Sasa nimeanza ku-focus kwenye maisha ya baadae baada ya kifo.
Maisha ni safari ndefu sana kijana wenu nimetimiza miaka 37 lakini mpka sasa mambo hayaeleweki

Sina moja au mbiliiiii
 

[emoji16] unanishaurije mim 26’s
 
Usikate tamaa, endelea kupambana, toka hapo ulipo nenda mji mwingine kapige kazi, usichague kazi kikubwa iwe ya halali.

Happy Birthday Bata Batani.
 
Tuseme huna hili wala lile..........hahahahahah! Pole mkuu, badli mfumo wa maisha. Na pia wacha kukata tamaa​
 
Bado dogo janja sana, una muda mwingi wa kuyapambania maisha yako.

Chamsingi ni kujua nini unacho kihitaji katika maisha yako.
Huo utajili na umasikini ni fikra zetu tu wanaadam.
 
Mkuu Umusolopogas hongera kwa kugonga nusu karne.
Si wengi miongoni mwetu watakaofika umri huo.
Nimepanda sana uamuzi wako wa kuanza kutafakari maisha baada ya kifo.
 
Asante mwanangu/mdogo wangu. Ni jambo la kumshukuru Mungu. Tuzidi kumtegemea.
Mkuu Umusolopogas hongera kwa kugonga nusu karne.
Si wengi miongoni mwetu watakaofika umri huo.
Nimepanda sana uamuzi wako wa kuanza kutafakari maisha baada ya kifo.
 
Mkuu huwezi kua na vyeti na mavitabu kibao alafu ukawa masikini.
Sema wewe bado hujakipata ukitakacho katika maisha yako.

Mkuu kuna watu hata mlo wa lakaa mbili unawashinda.

Kuna watu wameshatimiza miaka 70 alafu hawana hata mtoto wala nyumba ya kuishi, tena unakuta na maradhi yameshaanza kumuandama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…