Siku ya Magonjwa ya Kitropiki yasiyopewa Kipaumbele (NTD), January 30, 2023

Siku ya Magonjwa ya Kitropiki yasiyopewa Kipaumbele (NTD), January 30, 2023

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
January 30 ya kila mwaka, dunia huadhimisha siku ya Magonjwa ya Kitropiki yasiyopewa Kipaumbele (Neglected Tropical Diseases) kama sehemu ya kuongeza ufahamu na jitihada za kuyatokomeza magonjwa haya.

Ni mjumuiko wa magonjwa 20 yanayoathiri zaidi ya watu bilioni 1 kwenye nchi za Kitropiki pamoja na Nchi maskini duniani ambazo hukabiliwa na ukosefu wa huduma bora za maji, usafi wa vyakula na mazingira pamoja na uwepo wa huduma duni za afya.

Huitwa magonjwa yasiyopewa kipaumbele kwasababu hayapo kwenye mijadala na ajenda kubwa za kidunia zinazohusu masuala ya afya, hupokea rasilimali fedha ndogo kwenye tafiti na udhibiti pia huambatana na unyanyapaa na ubaguzi kwa wahanga hivyo ambayo kudhoofisha na hatimaye kuathiri ushiriki wa shughuli za kiuchumi na kijamii.

Baadhi ya magonjwa hayo ni Trakoma, Chagas, Ukoma, Dengu, Chikungunya, Matende, Kichaa cha Mbwa, Ngirimaji, Malale, Minyoo ya tumbo, Kichocho na Usubi.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) mabadiliko ya tabianchi nayo yamebadili mwelekeo wa magonjwa hayo na kuyafanya yaenee hata kwenye nchi zisizo za kitropiki.

Kwa pamoja, tunaweza kusaidia kujikinga na kudhibiti magonjwa haya kwa kutumia maji safi na salama pamoja na kutunza usafi wa mwili, mazingira na vyakula. Pia, matumizi ya dawa maalum (Preventive chemotherapy) kama sehemu ya kinga hufaa kwenye maeneo yaliyoathirika zaidi.

Chanzo: WHO
 
Back
Top Bottom