Siku ya Mashoto Duniani: Wana JF wenzangu tunaotumia mkono wa kushoto tukutane hapa

Kwa asilimia kubwa watu tunatumia mashoto tumepitia changamoto nyingi kuanzia shuleni lakini mimi namshukuru Mungu pamoja na dharau zote nilizipitia huko nyuma bado natumia mkono kwa mashoto mpaka sasa asante kwa mada nzuri barafu tupo pamoja
 
Asante sana mkuu barafu kwa mada maridhawa!
Mi mwenyewe mashoto!
Nakumbuka utotoni Baba alinipiga sana nisitumie mashoto hadi pale Mama alipoingilia kati.
Kuna siku tulizinguana na girlfriend wangu hotel pale niliposhika uma na kisu inversely na mazoea ya watu wengi akidae eti namtia aibu!!

Nimesoma uzi huu wote na >98% ya tabia zote za wenye mashoto ni sahii make ndo ninavyo behave hata mimi!
 
Mashoto wengi tumepitia 'treatment' mbaya wakati wa utoto tukilazimishwa kutumia mkono wa kulia. Let it be known that this is diversity of creation.
Kwa nchi zetu inatokana na kwamba mkono wa kushoto kwa ajili ya uchafu hivyo mtu analazimishwa mpaka inakuwa kero
 
Mada Yako inanishawishi nimuache mwanangu mwenye m iaka Miwil aendelee n.a. kutumia kushoto nikimpa pen anashika kushoto Mpira anapiga mguu wa kushoto .nilitaka kumbadil Lakin namuacha maana hat a mdogo Wangu wa kike n mashoto
 
Mm ni "mashoto". Nilibezwa sana na hali hii lakini nilkuwa najikubali. Yaani tokea utoto nilkuwa najikubali na naona fahari kuwa tofauti na wenzangu. Kipindi naanza shule ya msingi nilitumia kushoto, kuna mwalimu alikuwa ananikataza nikawa nabadili mikono. Akija kuniangalia natumia kulia akiondoka naanza mashoto. Mkono wa kulia ulizoea ila ulikuwa slow sana ktk kuandika kwahyo nikakomaa na mashoto mpk leo.
Nilipofika form four nakumbuka karibu robo ya darasa letu lilikuwa na mashoto na kufanya darasa kuwa na mashoto wengi kuliko darasa lolote lile ktk shule hyo.

Kilichokuwa kinanishangaza ni kwamba kwenye daftari nilikuwa nakuwa slow sana nikitumia mkono wa kulia hvyo lazima nitumie MASHOTO ila nikipewa kazi ya kuandika ubaoni mashoto ilkuwa slow sana hvyo kunilazimu kutumia mkono wa KULIA. Hili jambo liliwachanganya wengi wasigundue haraka natumia mkono gani.

Sjawahi kujutia kuwa "mashoto"
 

Mkuu inawezekana utafiti wako ukawa kweli kwa asilimia kubwa. Hapo umenigusa no 1 na 4!
 
Tupeni uhalisia wa maisha yenu je ni kweli mpo vizuri kimaisha kuliko wanaotumia kulia...!!
 
Leo ni siku ya watu wanao tumia mkono wa kushoto duniani. Inasheherekewa dunia nzima. Hivyo kama upo humu tusheherekee pamoja kwa kukomenti chochote juu ya changamoto na faida za kutumia mkono wa kushoto kwa jamii zetu za kitanzania.
Kwa upande mwingine watu wanaotumia mkono wa kushoto wamebarikiwa sana hii ni list tu ya baadhi ya watu mashuhuri wanao tumia mkono wa kushoto.
Barack obama
George .w. Bush
Billgates


Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkono wa mavi huo naona mnapeana moyo apa wakati kwenye familia zenu uko mnatumia kulia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…