Siku ya Mashoto Duniani: Wana JF wenzangu tunaotumia mkono wa kushoto tukutane hapa

Kama mimi tu. Kuna bibi mmoja wa jirani alinichapa sana kwa kutumia huu mkono
 
Dah ....Mie sioni tofauti yoyote kwenye mikono yangu ila mguu wa kushoto ndiyo napenda zaidi kuutumia ..[emoji124] [emoji124]
 
Naomba maelezo ya hiyo picha
Kwa ninavyojua yule anaetumia mkono wa kulia ubongo wake wa kushoto ndio unanguvu and vice versa
 
Kwenye hilo la kukosa usingizi linanikabili muda mwingi, mpaka huwa najiuliza ni nini tatizo?
Kwenye suala la wanyama, paka ni kati ya wanyama ninao wachukia sana. Ila Simba ndie ninayemkubali kuliko wote.
 
Mashoto wengi tumepitia 'treatment' mbaya wakati wa utoto tukilazimishwa kutumia mkono wa kulia. Let it be known that this is diversity of creation.

Naunga mkono %100 kuhusu mistreatment. Mimi nilivurugwa mno kiasi kwamba hadi leo nimebaki na imani tu kuwa mkono wangu wa kushoto ndio ninaoutegemea. Ila ukiniona ninavofanya shughuli zangu unaweza ukanihurumia

Mfano, nafua kwa mkono wa kushoto ila nakamua nguo kwa mkono wa kulia. Natupa mawe kwa mkono wa kushoto ila tenis nacheza na mikono yote. Yani huwa natamani nimletee noma aliyesababisha ila basi tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…