Siku ya Mashoto Duniani: Wana JF wenzangu tunaotumia mkono wa kushoto tukutane hapa

Ila vyengine inabidi ujifunze kama kutum

Na mimi mpaka kula ila najaribu sana kujiwezesha kutumia kulia kwenye kula
Nikiwa na waislam najitahidi kuitumia mkono wa kulia japo inakuwa tabu vibaya
 
Kwa wale wazee wa kupiga mkono, sipati picha mashoto anapigaje ile mambo. Ila nilitamani sana kuwa mashoto enzi za utotoni.
 
Mimi ni mashoto mpaka kula, na ni kweli hata wakati nasoma nilikuwa nasikiliza tu bila kuandika na sikuwahi kufeli
 
Nawashukuru sana wazazi na walimu wangu ambao hawakunizuia kutumia mkono wa kushoto kufanyia kazi,ila nakumbuka watoto wenzangu walinitesa sana kwa kunitenga wakati wa kula ktk sinia
 
nawaza tu huko toilet mkono unaohusika ni upi
 
Mashoto tupo. Baada ya kupita changamoto za utotoni tunaendelea na mashoto yetu kwa kwenda mbele. Kwa wale wanaokwazika kwa matumizi yangu ya mashoto poleni, ila ndio siachi.
 
wakati naanza shule nilikua naandika kutumia mkono wa kushoto,mwalimu wangu marehemu mama Mwingira(R.I.P) ligula priamry school enzi hizo alikua ana nichapa niache kutumia huo mkono dah nilipata shida sana.bahati nzuri mpk leo naweza kuandika kwa kwa kutumia mikono yote kushoto na kulia..
 
Najivunia kuwa mashoto, hata mwandiko ni safi tu hakuna shida
 
Asante sana kwa mada nzuri, hata mimi pia ni left hander, kuna nakala fupi nilikuwa nimeiandika naona mods wameitupa kapuni. Kama hawatajali bora waiunganishe na hii.
Nami pia mkuu na nimeandika kitu. Nashauri mods waziunganishe tu.

Kaka ...
 
Pole sana. Hayo ni moja ya madhila yanayowakuta watoto mashoto. Tuyakemee. Nimeanza mchakato wa kuwa na klabu ya mashoto Tanzania. Tujiuge pamoja kukuza uelewa mashoto so laana wala si dhambi.

Kaka ...
 
Pole sana, mimi mwanangu nimemlazimisha aandikie mkono wa kulia, sasa anaandikia yote.
 
Ukipigana na mwenye mashoto hakikisha mkono wa kushoto humpi nafasi ya kurusha ngumi uone atakavyohangaika ila usiombe akakubahatisha ngumi huwa nzito kama jiwe
Faida yetu ni kuwa sio wagomvi. Binafsi nimewahi kupigana mara moja katika maisha yangu mpaka sasa na hiyo ilikiwa darasa la 4 au 5. Ila kilichompata hiyo ndugu niliyepigana naye ...!

Kaka ...
 
Nimefurahi kukutana na wenzangu.

#HappyInternationalLefthander'sDay#
Kumbe na wewe pia, mimi mdogo wangu alipata shida, uelewa ulikuwa mdogo kipindi hicho, tulimfungia chura mkononi ili aache kutumia left hand, japo kula aliweza kutumia right hand lakini mengine hakuweza. Acha nikamtake radhi maana mimi ndiye nilikuwa kimbelembele cha kumkamata ili afungiwe chura.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…