Siku ya Mashoto Duniani: Wana JF wenzangu tunaotumia mkono wa kushoto tukutane hapa

Mimi mwalimu wangu alinizuia kuandikia kushoto. Dah mpaka sasa mwandiko wangu sio mzuri. Lakini kazi zingine zote natumia kushoto.
 
Nawashukuru sana wazazi na walimu wangu ambao hawakunizuia kutumia mkono wa kushoto kufanyia kazi,ila nakumbuka watoto wenzangu walinitesa sana kwa kunitenga wakati wa kula ktk sinia
Nami pia. Kudos kwa Mwalimu Mtawali!

Kaka ...
 
Pole kwa mdogo wako!


Kaka ...
 
Kiukweli kipigo nilikipata sana kuanzia nyumbani hadi shuleni,
Nyumbani hawakutaka kunielewa hasa kwenye kula,
shule waliniweza kwenye kuandika sema wameniharibu nina mwandiko kama bata kapita...

Ila imenisaidia baada ya kukua ukichanganya na mambo ya dini ndio kidogo naweza kujicontol kwa baadhi ya vitu.

Ukamuombe radhi mdogo wako, wallah ulikua unamkosea jamani.
 
Nishakusamehe ndugu.
 
Daah!! Nami pia ni mashoto nimepitia wakati mgumu sana katika maisha yangu kwasababu ya huu mkono wangu. Katika familia yangu tunaotumia mkono wangu kushoto tuko watatu kati ya kumi na mbili, mama, Dada na Mimi.
Kwasababu ya kupigwa ni wakati Wa kula tu ndo natumia Julia ila nikiwa natumia kijiko natumia kushoto. Mara nyingi wasionijua wananiona Wa ajabu.
Pia Niko vizuri sana katika kulenga shabaha, my dream ni kuwa sniper, my be one day yes.
 
Mimi enzi za vidudu hakukuwa na chekechea, tulianza kwa kuandika chini, nilikuwa naandika haraka kwa mkono wa kushoto halafu nabaki nimetegesha mkono wangu wa kulia kumhadaa mwalimu wangu ili asinipige.
Na nilikuwa watu wa mwanzo kabisa kuruhusiwa kutumia kalamu ya wino tulipofika darasa la tatu kwasababu nilikuwa na mwandiko nzuri. Nimewakilisha shule yangu nilipofika darasa la nne kwenye shindano la mwandiko umitashumta.
 
Ujue utoto kazi Sana.. Mimi na yeye tumezaliwa kwa kufuatana, ugomvi ulikuwa hauishi...

Kwa hiyo alikuwa akifanya kitu kwa mashoto, mimi ni wa kwanza kuripoti ili apigwe...
Na fimbo naandaa kabisa naificha, ikitakiwa naichomoa fastaa.. Halafu namkimbiza namkamata namuwasilisha kwa pilato..

Kuna chura alikamatwa akafungwa chini ya mchungwa home...
Nilimnyanyasa sana dogo, kila saa namkamata nampeleka kwenye chura, ilibidi chura afunguliwe kwa sababu nilimtumia kama silaha.

Akipewa chochote cha kula namtisha kumletea chura ananipa, then mimi ndio namgawia kidogo.. Mama alipojua huo ukuda alinipa kichapo cha paka mwizi.

Utoto una mengi..
 
Mashoto wengi wanakuwaga villaza sijui kwa nini?
 
Wow! Utoto raha jamani,
Mimi niliefatana nae ni wa kiume, alikua mnoko kama ulivyokua wewe yan [emoji1] ,

Mama asipokuwepo maisha kwangu yalikua magumu sana, ila siku moja katika kunionea kwake, nilichukua msukumio wa chapati nilimpiga nao sana hata sijui nguvu zilitoka wapi, (Miracle of left hand) hehehe tangu siku ile heshima na adabu mpaka leo watu wazima na ndio tumekua tunapendana hatari.

Lakini wewe ulikua mkorofi sana jamani, mpk wamtishia chura ili akupe kitu, duuuh!
 
Mwalimu wa chekechea alimlazimisha mtoto wangu kuandikia mkono wa kulia.
Mtoto alikuwa anatumia mkono wa shoto nakubaliana na wewe ni mchoraji mzuri sana hata kichwani yupo vizuri ktk masomo.
 
Acha tu ndugu yangu, pona yake ilikuja nilivyokwenda boarding school, halafu baada nikawa Nam miss kweli, nikirudi likizo nikawa namnunulia vizawadi, kuanzia hapo na akili yangu ikawa imepevuka nikaacha ukorofi. Kwa sasa ndo shost na msiri wangu.
 
Acha tu ndugu yangu, pona yake ilikuja nilivyokwenda boarding school, halafu baada nikawa Nam miss kweli, nikirudi likizo nikawa namnunulia vizawadi, kuanzia hapo na akili yangu ikawa imepevuka nikaacha ukorofi. Kwa sasa ndo shost na msiri wangu.
Watoto wa kufatana lazima wawe wanagombana na kuna wengine hugombana mpaka ukubwani, lakini hapo hapo wanapendana.

Mpe hai shost ako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…