Siku ya Mashoto Duniani: Wana JF wenzangu tunaotumia mkono wa kushoto tukutane hapa

Yerewiiiiiiii Mimi pia ni mashoto lakini baba angu hakufurahia Mimi kula na kuandikia kushoto hivyo alihakikisha nakula nae sahani moja na kun in yang'anya chakula endapo nitakichukua kwa mkono wakushoto lakini bado haitoshi alijitoa muda wake wa jioni kunifundisha hesabu na akawa ananisimamia nikiwa naandika anipokonya kalamu nikiishikia kushoto...mpaka Leo Mimi naandikia kulia lakini bado kushoto naandikia pia.na kupika kufua na kuosha vyombo natumia kushoto tuuu.
 
Daaaaah!! Nilimiss hii but tuko pamoja! Am happy kutumia mashoto.
 
Haaaaa na hiii ipo nimemkumbuka kaka yangu anaitwa KEMA ana shoto anaitumia kisistaarabu wacha shabaha kama snipper
 


Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app
 
Mtoto wangu wa kwanza ni mashoto.
Wakati anaanza shule ya awali nilikuwa napata tabu sana kumshikisha penseli wakati wa ku trace/kuandika. Na ikawa inanibidi nimshikishe wa kulia.
Ila ukimwacha tu kuandika mwenyewe anarudi kwa ule ule wa shoto.
Hadi leo anatumia mashoto kwa kila kitu tena ni mchoraji mzuri sana.
Sema wakati mwengine anaandikia kulia pia, tena muandiko wake ni mzuri kwa mikono yote miwili.
Anapenda sana mambo ya art na design
 
Tupo wengi sana...mimi yananihusu mambo mengi kweli katika hayo uliyoyasema
1.Aleji hapa ndio nyumbani kwao
2.Hapa nilipo nina fanya shughuli tatu kwa pamoja za kila siku
3.Huwa siwazi kitu kwa zaidi ya saa 12 halafu nikashindwa kupata ufumbuzi,hata jambo liwe gumu vipi lazima nitatafuta Suluhisho tu...tena suluhisho bora.
4.Nina hisia sana,kulia kwangu ni kitu cha haraka zaidi,hata nikiwa na furaha basi huwa nalia(ujinga wa hali ya juu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23])
5.Huwenda pia kifo changu kikatokana na ajali maana mara nyingi nasahau alama za barabarani hasa kwenye mataa,kawaida yangu kupinda kushoto...nina kesi nyingi za ajali (naogopa katika hili[emoji22][emoji22])
 
Tabia zote ulizataja ninazo, pia napata shida kwa habari ya kuendesha magari. Kwa sasa natumia mikono yote sawa sawa ina uzito sawa baada ya kuambiwa wa kushoto wa shetani nikiwa mdogo najifunza kuandika hivyo nika adopt kutumia kulia baadhi ya kazi.
Nina alergies
Nilishakuwa na insomnia.
Nimeweza kuwa mchoraji, nimewahi kuandika mashairi pia, uandishi mbali mbali hata nikatunukiwa vyeti nikiwa kidato cha nne. pia nimepursue science studies...ingawa walimu wangu wa masomo ya arts o level walinitaka niwe mwandishi maana mwalimu wangu wa kiswahili alikuwa mhariri wa vitabu na aliniita aliposikia nafanya mtihani wa physics kidato cha nne akaniuliza nataka nini, mbona napoteza uelekeo! ?
Sasa nasema God's grace can take you places where your talents can't.
Katika biblia Benjamini alikuwa mashoto, tusiwatese watoto kuadopt mikono ukubwan tunaishia kuwa both handed hali inayosumbua kutafsiri upande ukitajwa maana mikono huwa na uzito sawa.
 
Umenikumbusha mbali sana wkt nilipokuwa na umri mdogo, wazazi wng pamoja na walimu shuleni walinichapa sana na kuufunga mkono wang wa kushoto ili tu niache kuutumia lkn ilishindikana. Kitu walicho faulu ni kunifanya niandikie kulia lkn mengine yote walifeli

Sent from my Y3S using JamiiForums mobile app
 
Nimecheka sana mkuu....nimeshawahi kushuhudia familia za namna hiyo hasa kwa watoto waliofatana..ni vita tu[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Masud Kipanya..atakua ni mashoto haya uliyo yazungumza hapa ana fananana nayo sana..Hebu watu wake wa karibu tujuzeni.!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…