Siku ya Mtoto wa Afrika: THRDC, LHRC -Watoto wengi bado wanapata shida ya huduma za maji safi na vyoo salama

Siku ya Mtoto wa Afrika: THRDC, LHRC -Watoto wengi bado wanapata shida ya huduma za maji safi na vyoo salama

News Tz1

Member
Joined
Nov 28, 2025
Posts
82
Reaction score
110
Historia inairejesha nyuma Afrika, mnamo tarehe 16 Juni 1976, ambapo maelfu ya watoto katika nchi ya Afrika Kusini walikusanyika katika mji wa Soweto kwa ajili ya maandamano yenye malengo ya kudai elimu bora,ambapo licha ya kuwa watoto lakini mamia ya watoto walipigwa risasi na kuuawa huku watoto zaidi ya elfu moja wakijeruhiwa.Tangu 1991 Jumuiya ya Umoja wa Afrika iliweka siku ya Watoto wa Afrika kila tarehe 16, June.

Katika kuadhimisha Siku hii leo Jene 16, 2026, Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kwa kushirikiana na wadau wengine wameadhimisha siku hiyo kwa kuwaleta pamoja watoto ikiwemo wenye ulemavu, ambapo wamefanya mjadala kuhusu umuhimu wa huduma za maji safi na vyoo salama.

Maadhimisho ya mwaka huu (2026) yamebebwa na Kaulimbiu isemayo: Kuhakikisha Upatikanaji wa Huduma za Maji, Usafi wa Mazingira naAfya kwa Kila Mtoto Barani Afrika.

Wakisoma tamko la pamoja wameeleza


Leo tunaungana na watoto wengine barani Afrika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika 2026. Siku hii inatukumbusha kuwa watoto wana haki ya kuishi kwa usalama, kupata elimu bora, afya nzuri na kuheshimiwa.

Mwaka huu tunazungumzıa umuhimu wa maji safi, vyoo bora na usafi wa mazingira kwa watoto wote. Watoto wengi bado wanapata shida ya maji safi, vyoo salama na sehemu za kunawia mikono, hasa mashuleni na vijijini. Hali hii husababisha watoto kuugua mara kwa mara, kukosa shule na kuishi katika mazingira yasiyo salama.

Maji safi na mazingira safi siyo zawadi, ni haki ya kila mtoto. Mtoto anapokuwa mgonjwa kwa sababu ya maji machafu au ukosefu wa usafi, anashindwa kusoma vizuri na kutimiza ndoto zake. Pia watoto wengi hutumia muda mwingi kutafuta maji badala ya kusoma na kucheza.

Watoto wenye ulemavu hukutana na changamoto kubwa zaidi pale ambapo vyoo na huduma za maji hazijajengwa kwa kuzingatia mahitaji yao. Hivyo, ni muhimu

kuhakikisha kila mtoto anapata huduma hizi bila ubaguzi." imeelezwa sehemu ya Tamko hilo


Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dkt. Anna Henga amesema kwamba changamoto ya upatikanaji wa maji salama inaathiri maisha ya watoto wengi kwenye hususani maeneo ya Vijijini.

Ametoa wito kwa Serikali kuchukua hatua za kutenga bajeti ya kutosha ili kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji na salama ili kuwalinda watoto na magonjwa yanayoweza kuepukika.

" Kuna Matukio utekaji wa watoto"

Pamoja na hivyo amesema kwamba bado kumeendelea kujitokeza matukio ya ukatili wa watoto ikiwemo utekaji, ambapo ametaja visa vya watoto watano kutekwa kwa nyakati tofauti katika kipindi cha Mwezi June 2026, ambapo wawili wamepatikana wakiwa hai huku wengine watatu waliodaiwa kutekwa mkoani Lindi amedai kuwa miili yao imeokotwa.


Amesema kuwa hatua za kuwakamata na kuchukulia hatua za kisheria watuhumiwa zinatakiwa kufanyika haraka, ambapo amedai kwamba hakuna taarifa za kukamatwa kwa wahusika wa tukio la watoto waliodaiwa kuwatekwa mkoani Lindi kabla ya miili yao kuokotwa.
 
Back
Top Bottom