KERO Siku ya pili Mtandao wa Vodacom upande wa M-PESA unasumbua sana

KERO Siku ya pili Mtandao wa Vodacom upande wa M-PESA unasumbua sana

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Airtel money yenyewe mara nyingi sana wanakuwa na Maintenance kuanzia saa sita usiku bila hata taarifa mpaka asubuhi, Upande wa uhakika wa malipo kwa Usiku ni Selcom Pesa
 
Siku ya pili mtandao wa vodacom upande wa MPESA unasumbua sana. Sisi wafanyabiashara na watu wanaoutegemea tunataabika sana. Alafu hayatoi taarifa wala nini.
Kama unatumia app ndo una shida ila menu ya kawaida inafanya kazi
 
Voda naomba mnirudishie hela yangu.Mngejua kuna tatizo mlipaswa kutuma mesej kwa wateja!
 
Hii mitandao ya simu ingekua inafanya hivi kwa watu wanaojitambua kama wazungu wangefilisika ndani ya mwezi tu kwa kilipa fidia kila uchwao huko kotini
 
Kuna hela hazionekani na namba ya huduma kwa wateja wameifunga. Inaonekana mifumo yetu ya kipesa inahackiwa sana.
 
Back
Top Bottom