Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari: Uandishi wa Habari bila Hofu au Upendeleo

Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari: Uandishi wa Habari bila Hofu au Upendeleo

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari maarufu kama Siku ya Waandishi wa Habari Duniani ni ni moja ya matukio yaliyopanga, kusimamiwa na kuhamasishwa na Umoja wa Maifa likiwa linaadhimishwa kila mwaka Mei 03

Siku hii inaadhimishwa kuongeza uhamasishaji kuhusu umuhimu wa uhuru wa waandishi wa habari. Ni siku ya tafakari kati ya Wataalamu wa Vyombo vya Habari kuhusu masuala ya uhuru wa waandishi wa habari na maadili ya kitaaluma

Mei 03 kila mwaka ni siku ya kuunga mkono Vyombo vya Habari vinavyolengwa ili zuzuiwa au kuondolewa uhuru wake wa kutoa taarifa. Pia, ni siku ya ukumbusho kwa waandishi wa habari waliopoteza maisha katika harakati za kutafuta taarifa

Kaulimbiu Kuu kwa siku ya siku ya leo ni "Uandishi wa Habari bila Hofu au Upendeleo", lakini kuna kaulimbiu ndogo ambazo ni; Usalama kwa Waandishi wa Habari wakike na wakiume pamoja na Wanyakazi wote wa wa Vyombo vya Habari

Kaulimbiu ndogo nyingine ni Uandishi wa Habari wa Kujitegemea na Utaalam huru kutoka kwa Ushawishi wa Kisiasa na Biashara na nyingine ikiwa ni Usawa wa Kijinsia katika nyanja zote za Uandishi wa Habari

Msuala yanayotishia taaluma ya habari mbeleni kama yalivyoainishwa na 'The 2020 World Press Freedom Index' ni Mzozo wa jiografia (Kwa sababu ya uchokozi baina ya Serikali za Kitawala); pamoja na Shida ya kiteknolojia (kwa sababu ya ukosefu wa dhamana ya Kidemokrasia)

Nyingine ni Shida ya Kidemokrasia (kwa sababu ya sera kukandamizi); Shida ya Kuaminiana (kwa sababu ya tuhuma na hata chuki dhidi ya Wanahabari); na Shida ya Kiuchumi (uboreshaji wa uandishi wa habari bora)
 
Tanzania hatuwezi kuazimisha siku hii kwa kuwa waandishi wengi wamenyongwa,wamepewa kesi za kuhujumu uchumi,kwa hiyo kwaTanzania tupo gizani yaani tupo shimoni ,wananchi wameambiwa wasikilize habari moja tu kwamba magufuli ametekeleza bila kujali ametekeleza kwa namna Gani.Leo hii huu ni mwaka wa tano chombo cha kufunga Sheria tena cha uwakilishi wa wananchi yaani BUNGE ,ni marufuku kuangalia labda wananchi waangalie saa 5:00 usiku tena baada ya kufutwa baadhi ya maneno ambayo walipakodi ilibidi wasikie kutoka kwenye vyombo vya habari lakini kwa Tanzania ni kama tupo Somalia kwa kweli kama waandishi wa habari wanakazi kubwa na nchi hii ,maana mtu aliyehitimu uandishi habari za uchunguzi awamu hii anawaza anawezaje kuchunguza habari !leo hii habari za kibiti zimefichwa,habari za kutupwa watu baharini zimefichwa ,leo hii watu wanazikwa usiku zimefichwa,leo hii bei za ndege mpya zimefichwa ,juzi Mzee Prince Bagenda amekamatwa kisa anaandika kuhusu utawala wa magufuli sasa huyu mwandishi wa bongo atakimbilia wapi?Yaani ugaidi juu ya ugaidi ,mateso juu ya mateso
 
Back
Top Bottom