Siku ya UKIMWI Duniani: Ushuhuda - Asante Hospitali ya Jeshi Lugalo

Siku ya UKIMWI Duniani: Ushuhuda - Asante Hospitali ya Jeshi Lugalo

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594
Wakati mwingine ukitazama nyuma ni lazima utashukuru Mungu kwa kupita kwenye tanuru la giza nene!

Huu mkasa ni wa kweli kabisa na naishukuru sana Hospitali ya Jeshi Lugalo kwa kuokoa maisha ya ndugu yangu ambaye aliponea chupuchupu kupoteza maisha.

Mkasa umetokea muda kidogo.

Ndugu yangu alizaliwa na kukua akiwa tayari ameathirika na kuthibitishwa kuwa an Virusi Vya Ukimwi (VVU). Hata hivyo alikuwa ameikubali hali hiyo toka utotoni na sasa anaenda miaka 30 hivi.

Anaishi akiwa amepanga mwenyewe na vijana wenzake na alikuwa anaendelea vizuri tu na kula dawa za kufubaza, na afya yake kwa nje inaonekana ni njema tu. Kosa akaacha kutumia dawa baada ya kuona afya imeimarika.

Siku mimi niko mishe mishe zangu nikapigiwa simu. "Hello, we ndiye ndugu yake nanihii?" Nikajibu "ndiyo", huku kiroho kikinidnda nikijiuliza kunani?

"Toka juzi hali na anaongea maneno hatuyaelewi, na alikuwa na homa, naona kama imepanda kichwani" Nikawaambia hao jamaa wa karibu nakuja sasa hivi ili nimwone.

Kweli nikawasha gari moja kwa moja ghetto yake na nikamkuta kwa kweli ana hali mbaya sana ambayo sikuwahi kumwona nayo.
Alikuwa sasa kama anapoteza fahamu na povu linamtoka mdomoni.

Kwa uzoefu wangu mjini nikaona mahali pa kumpeleka bila urasimu na kwa haraka ni Lugalo General Military Hospital na nikapiga spidi mpaka hapo.

Kwa kweli nawashukuru sana madaktari na manesi pale, nikawaeleza historia ya mgonjwa kuwa ana VVU na kwamba sasa amepta homa inyomuendesha na amepoteza fahamu.

Kitu cha kwanza kilikuwa kucheki mapigo ya moyo yanaendaje, na akapewa huduma ya kwanza.

Wale madaktari, tena wamevaa kijeshi, walimhudumia bila kunyanyapaa wala kusita. Mgonjwa wangu alikuja kuzinduka baada ya masaa 24 huku tukiwa na wasi wasi mkubwa.

Hatimaye mgonjwa akazinduka na hakujua yuko wapi. Alichokumbuka mara ya mwisho ni kuwa na rafiki zake kule anakokaa.

Na hata baada ya hapo mgonjwa aliendelea kupata matibabu ya kurudisha hali yake ya kawaida kwa muda wa wiki tatu pale Lugalo.
Kumbe mwili ulikuwa umepigika sana na viungo muhimu vilikuwa vina-perform chini kabisa ya uwezo wake.

Kwa kweli tulimshukuru Mungu na hasa wale vijana wenzake waliotoa tahadhari na kutupigia simu kueleza hali ya mgonjwa, maana wangezembea tu kutoa taarifa mgonjwa wetu angekuwa historia.

Madaktari na manesi hadi wahudumu, Lugalo General Military Hospital mubarikiwe sana.
 
Ukimwi unaua na bado ni ugonjwa unaotisha duniani zaidi ya miaka 40, jambo la msingi tuache ngono ndio chanzo kikuu, tamaa ya ngono, ukimwi unatesa sana kuliko hata maradhi mengine.

Ukimwi hauna Kinga wala tiba.
 
Kabla hujaupata, UKIMWI ni hatari sana jihadhari na ujikinge kwa gharama yoyote.

Ukishaupata, UKIMWI ni ugonjwa wa kawaida tu kama magonjwa mengine. Unaweza kuishi tena bila wasiwasi wowote!

Akili kumkichwa.[emoji1493][emoji1493][emoji1493]
 
Kabla hujaupata, UKIMWI ni hatari sana jihadhari na ujikinge kwa gharama yoyote.

Ukishaupata, UKIMWI ni ugonjwa wa kawaida tu kama magonjwa mengine. Unaweza kuishi tena bila wasiwasi wowote!

Akili kumkichwa.[emoji1493][emoji1493][emoji1493]
Tatizo ukipuuzia masharti yake ni hatari sana na unaweza ondoka duniani bila kuaga.
 
Ukimwi unaua na bado ni ugonjwa unao tisha duniani zaidi ya miaka 40, jambo la msingi tuache ngono ndio chanzo kikuu, tamaa ya ngono, ukimwi unatesa sana kuliko hata maradhi mengine.
Ukimwi hauna Kinga wala tiba.
Kinga ya ukimwi sii kutokugegeda
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Tatizo huo ugonjwa umekaa pabaya mkuu.
Ingekuwa huo ugonjwa unapatikana kwenye ugali watu tungeachana na ugali hata mahindi yasingelimwa kabisa.
Vijana wanapataka wazee wanapata🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Hapo ndio tatizo.
Halafu wazee wanatengeneza misemo yao ya utetezi eti wanasema "ng'ombe hazeeki maini"
Hapo ndipo vurugu zinapoanzia na ndio maana ukisema uchukue binti mdogo ukamwamini unakwenda na maji kwa sababu wazee wanapitia wote.
Vijana wanapataka wazee wanapata[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Eeeeeh...
IMG-20201201-WA0004.jpg
 
Kwa nini wenye virusi vya ukimwi hawataki kujitangaza juu ya halimzao??!!!
Kama wenye maambukizi wataamua kujiweka wazi basi itasaidia sana kupunguza maambukizi au waweke chapa kuwa huyu ni mwathirika ili jamii imtambue
 
Zamani wenye virusi vya ukimwi walikuwa wanafahamika Kwa mwonekano kama vile; ukondefu, vidonda nk, lkn sasa huwezi kumtambua, mimi nashauri Madaktari watoe taarifa za waathirika ili wajulikane
 
Vijana wanapataka wazee wanapata[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Unaweza ukala bila kunawa ukimaliza sasa unaanza kuwaza sijabeba maradhi kweli
 
Kumbe bado Tanzania tuna Madaktari wa ukweli na manesi? Lugalo Hospital kwa kweli mbarikiwe sana kwa hili.
Kwa kweli mkuu, huyu ndugu yetu alipata matibabu bila unyanyapaa wala dharau.
Wote walikuwa waki sypamthise.
Hatuna cha kuwapa ila kuwaombea mema kwa Mola.
 
Kwa nini wenye virusi vya ukimwi hawataki kujitangaza juu ya halimzao??!!!
Kama wenye maambukizi wataamua kujiweka wazi basi itasaidia sana kupunguza maambukizi au waweke chapa kuwa huyu ni mwathirika ili jamii imtambue
Tatizo jamii zetu zina uelewa mdogo kuhusu ukimwi.
Mtu akijitangaza wanamnyanyapaa na kumnyooshea vidole kila apitapo hapo ndio tatizo linapoanzia
 
Tatizo jamii zetu zina uelewa mdogo kuhusu ukimwi.
Mtu akijitangaza wanamnyanyapaa na kumnyooshea vidole kila apitapo hapo ndio tatizo linapoanzia

Sasa na wewe kwa nini ujisikie vibaya kama unaikubali hali yako ya maambukizi, fahamu kuwa kunyanyapaliwa ni sehemu ya changamoto kamwe hazito isha, unapaswa ukubaliane nazo sio kuogopa kujitangaza, jitangaze ili uwanusuru wwngine, tutapendekeza mswaada wa sheria kila mwathirika lazima atangazwe au atambuliwe na jamii iliyo mzunguka
 
Back
Top Bottom