Siku ya UKIMWI Duniani: Ushuhuda - Asante Hospitali ya Jeshi Lugalo

Siku ya UKIMWI Duniani: Ushuhuda - Asante Hospitali ya Jeshi Lugalo

Sasa na wewe kwa nini ujisikie vibaya kama unaikubali hali yako ya maambukizi, fahamu kuwa kunyanyapaliwa ni sehemu ya changamoto kamwe hazito isha, unapaswa ukubaliane nazo sio kuogopa kujitangaza, jitangaze ili uwanusuru wwngine, tutapendekeza mswaada wa sheria kila mwathirika lazima atangazwe au atambuliwe na jamii iliyo mzunguka
Mkuu ni hivi,wakitangazwa maana yake hata nyumba za kupanga watakuwa wanakosa.
Yaani hata wenye nyumba watakuwa wanawakatalia kupanga,huo ndio uelewa wa jamii yetu huwa wanadhani ukimsogelea tu mwathirika anakuambukiza
 
Kuna manzi moja nilikula nakumbuka ilikua ijumaa usiku aise jumamosi asubui nikakuta mb... Yangu inauma balaa nikajikaza kiume bwanae siku ya pili maumivu yalizidi nikienda haja ndogo damu inatoka na maumivu makali adi nilikua natoa machozi. Aise nikamkubuka yule manzi nikawaza hii ni UTI bila Shaka siku ya nne nikakuta usaa unatoka palepale nakaenda hospital nikapewa dawa nikatumia ndani ya siku mbili nikawa fiti.
NB;mm nilichowaza zaid nilihisi ameniachia na ukimwi hili ndo kilinipa stres acha
 
Wakati mwingine ukitazama nyuma ni lazima utashukuru Mungu kwa kupita kwenye tanuru la giza nene!

Huu mkasa ni wa kweli kabisa na naishukuru sana Hospitali ya Jeshi Lugalo kwa kuokoa maisha ya ndugu yangu ambaye aliponea chupuchupu kupoteza maisha.

Mkasa umetokea muda kidogo.

Ndugu yangu alizaliwa na kukua akiwa tayari ameathirika na kuthibitishwa kuwa an Virusi Vya Ukimwi (VVU). Hata hivyo alikuwa ameikubali hali hiyo toka utotoni na sasa anaenda miaka 30 hivi.

Anaishi akiwa amepanga mwenyewe na vijana wenzake na alikuwa anaendelea vizuri tu na kula dawa za kufubaza, na afya yake kwa nje inaonekana ni njema tu. Kosa akaacha kutumia dawa baada ya kuona afya imeimarika.

Siku mimi niko mishe mishe zangu nikapigiwa simu. "Hello, we ndiye ndugu yake nanihii?" Nikajibu "ndiyo", huku kiroho kikinidnda nikijiuliza kunani?

"Toka juzi hali na anaongea maneno hatuyaelewi, na alikuwa na homa, naona kama imepanda kichwani" Nikawaambia hao jamaa wa karibu nakuja sasa hivi ili nimwone.

Kweli nikawasha gari moja kwa moja ghetto yake na nikamkuta kwa kweli ana hali mbaya sana ambayo sikuwahi kumwona nayo.
Alikuwa sasa kama anapoteza fahamu na povu linamtoka mdomoni.

Kwa uzoefu wangu mjini nikaona mahali pa kumpeleka bila urasimu na kwa haraka ni Lugalo General Military Hospital na nikapiga spidi mpaka hapo.

Kwa kweli nawashukuru sana madaktari na manesi pale, nikawaeleza historia ya mgonjwa kuwa ana VVU na kwamba sasa amepta homa inyomuendesha na amepoteza fahamu.

Kitu cha kwanza kilikuwa kucheki mapigo ya moyo yanaendaje, na akapewa huduma ya kwanza.

Wale madaktari, tena wamevaa kijeshi, walimhudumia bila kunyanyapaa wala kusita. Mgonjwa wangu alikuja kuzinduka baada ya masaa 24 huku tukiwa na wasi wasi mkubwa.

Hatimaye mgonjwa akazinduka na hakujua yuko wapi. Alichokumbuka mara ya mwisho ni kuwa na rafiki zake kule anakokaa.

Na hata baada ya hapo mgonjwa aliendelea kupata matibabu ya kurudisha hali yake ya kawaida kwa muda wa wiki tatu pale Lugalo.
Kumbe mwili ulikuwa umepigika sana na viungo muhimu vilikuwa vina-perform chini kabisa ya uwezo wake.

Kwa kweli tulimshukuru Mungu na hasa wale vijana wenzake waliotoa tahadhari na kutupigia simu kueleza hali ya mgonjwa, maana wangezembea tu kutoa taarifa mgonjwa wetu angekuwa historia.

Madaktari na manesi hadi wahudumu, Lugalo General Military Hospital mubarikiwe sana.
Pamoja na udogo wa hospitali, Lugalo imejipatia sifa sehemu nying kwa uadilifu na weledi kidaktari.
Pia wana clinical care nzuri sana ukilinganisha na hospitali za kawaida za serikali.
 
Kwa nini wenye virusi vya ukimwi hawataki kujitangaza juu ya halimzao??!!!
Kama wenye maambukizi wataamua kujiweka wazi basi itasaidia sana kupunguza maambukizi au waweke chapa kuwa huyu ni mwathirika ili jamii imtambue
Kuna muda unasoma utumbo kama huu unajiuliza hivi duniani kuna wapumbavu wa kiwango hiki?
 
Back
Top Bottom