Uchaguzi 2020 Siku ya uzinduzi wa kampeni kwa upande wa CHADEMA Dar es Salaam kutafurika umati wa watu haijawahi kushuhudiwa tangu tupate Uhuru

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Wakuu kwema!

Siku ya uzinduzi wa kampeni, siku ambayo Mh. Tundu Antipas Lissu atatema madini adimu bila kumung'unya maneno.

Mimi binafsi nitahudhuria, umati utakaoshuhudiwa siku hiyo utakuwa mkubwa sana. Watumishi walioongopewa mishahara minono watatoroka kazini kwenda kupata tumaini, wafanyabiashara walioteswa na TRA watafunga biashara zao kwenda kula neno la tumaini.

Vijana waliokosa ajira ambao wengi wako hapa Dar es Salaam hawatakosa.

Itakuwa aibu kubwa kwa CCM, chama ambacho rushwa ni halali. CCM nao watawazoa wajumbe na UVCCM kwa ujira wa elfu tano ili wakasikilize mambo ya ununuzi wa Bombardier, SGR na viwanda zaidi ya elfu 8 na ajira hewa zaidi ya milioni sita.

Najua wapo watakaokuja na kauli za umati wa mikutanoni si kitu. Lakini mutambue kuwa CHADEMA haisombi watu kwa malori kisha kuwalipa sahani ya ubwabwa na sh.elfu tano, watu wataacha kazi zao willingly ili wakamsikilize watakayempigia kura mheshimiwa Lissu ambaye hatumii nguvu kujibrand.

Kama umati sio issue mbona akina johnthebaptist na wenzake wanateseka kila wanapoona Lissu analakiwa kama mfalme kila anakokwenda!
 
Mkuu kwa jicho la tatu kujazana kwenye kampeni sio kupiga kura.

Tuhamasishane siku ya kupiga kura tuende kwa wingi ili ushindi uwe mnono.

Kuwa wengi kwenye kampeni ni kuwa tunakusanyika kwa wagombea wote ili tusikikize sera na kuzipima kama zinatufaa.
 
Kuna msemo kuzikwa na watu wengi sio kwenda peponi
 
Mkuu kwa jicho la tatu kujazana kwenye kampeni sio kupiga kura.

Tuhamasishane siku ya kupiga kura tuende kwa wingi ili ushindi uwe mnono.

Kuwa wengi kwenye kampeni ni kuwa tunakusanyika kwa wagombea wote ili tusikikize sera na kuzipima kama zinatufaa.

Kama ni sera wanataka kusikia, mbona hawajazani kwa Hashimu Rungwe?
 
Inafutana anapo zindua kampeni zake amezungumza nini

Mfano kwa sasa anazungumzia ubwabwa na kubeti sijui nan ataenda kusikiliza hizo sera

Kuna wakati unaangalia sera za mgombea nk nini na ni wakat gan
 
Umpende usimpende, umpe kura usimpe, ashinde asishinde siasa za Tanzania hazitakua zile zile -zitabadilika.
Tuombe tu TV na Radio wawe wavumilivu na wasiwe waoga. Tumeona Lissu akizungumza basi inakuwa shida mitambo inagoma. Kumbuka 2015 mitambo ya TBC ilikwama (Marehemu Marin Hassan Marini na bosi wake Tido). Sasa subiri Lissu akinguruma.
Watanzania tumezoea kuita "chepe" kuwa ni "kijiko" na mtu akisema chepe ni chepe basi tunamsingizia ketukana. Enzi za chama kimoja zimepita tuwe tayari kuelezana ukweli na kukosoana.
 
Acha ujinga tafadhali, ameongea mambo mengi ya maana, ila watu wameripoti zaidi hilo la kubet na ubwabwa. Acha kukaa huku mitandaoni na kupewa habari za kuokoteza, kisha uanze kuzijengea hoja.
 
Uko sahihi kabisa. Eti Makada wa ccm ndio wanapanga jinsi ya wapinzani kufanya siasa, wanasema usimseme mtu au kumshambulia, bali uwaeleze wananchi utawafanya nini. Wasikilize huko US kwenye demokrasia za ukweli jinsi Trump anavyoshambuliwa. Unafanyaje siasa bila kutaja mapungufu ya mshindani wako.
 
Nimekwambia mfano sijui kama unaelewa maana ya mfano

uwe unasoma na kwelewa ndipo umshambulie mtu usiseme mjinga wakat hujaelewa alicho andika
 
Uko sahihi kabisa. Eti Makada wa ccm ndio wanapanga jinsi ya wapinzani kufanya siasa, wanasema usimseme mtu au kumshambulia, bali uwaeleze wananchi utawafanya nini. Wasikilize huko US kwenye demokrasia za ukweli jinsi Trump anavyoshambuliwa. Unafanyaje siasa bila kutaja mapungufu ya mshindani wako.
Mgombea mzuri lazima ajue mapungufu ya mpinzani wake ili amuanike. Baada ya miaka mitano ya kujipigia upatu,upinzani utakuwa na miezi miwili tu ya kujieleza. Na kujieleza kwao ni pamoja na kuonyesha mapungufu gani makubwa (tactical and strategic ) yamefanywa na upande wa pili na wao wana dawa gani. Pia ni kitu gani wanaweza kufanya cha ziada kuendana na wakati.
I hope ukiacha mikutano watakuwa pia wananunua airtime wazungumze na watanzania moja kwa moja.
 
Back
Top Bottom