Siku ya WAKUNGA Duniani

Siku ya WAKUNGA Duniani

Page 94

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Posts
5,204
Reaction score
15,207
Salaam Wakuu,

Leo ni siku ya Maalum kabisa kwa watu muhimu sana katika nyanja ya afya duniani. Siku ya WAKUNGA.

Kila mmoja wetu hapa huenda Wakunga wamechangia kwa kiasi kikubwa ili kufikia katika mikono Salama.

Wakunga wawe wa jadi au waliofunzwa ni watu maalum sana katika maisha yetu. Huhimili vitu vingi katika kumpokea kiumbe kipya duniani.

Mimi binafsi nina Shukrani kubwa sana kwa wakunga hasa Wakunga wa jadi. Huenda leo nisingelikuwepo kama siyo jitihada zao katika kufanikisha kuwa nakuwa hai.

Walitumia maarifa na jitihada zao kadri wawezavyo ili kufanikisha maisha yangu yanasonga mbele. Ijapo nilimpoteza mama yangu (pumzika kwa amani), lakini mimi nilipona na sasa nahimili ya Dunia. Isingelikuwa jitihada zao, huenda leo JF isingelikuwa na michango wala nisingelitambulika humu.

Hakika ni jitihada za Kupongezwa na kushukuriwa kulikopitiliza. Mungu awajalie mema na mazuri sana Wakunga wetu wa jadi na hawa waliofunzwa....

One way to measure a particular doctor's openness and attitude toward women in general is simply to ask about the doctor's opinion of midwifery.

Je, wewe una nini cha kuwaambia Wakunga katika siku yao Maalum?
 
Back
Top Bottom