Siku ya wanawake duniani: Balozi Ami Mpungwe azungumza

Siku ya wanawake duniani: Balozi Ami Mpungwe azungumza

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Baada ya kumsoma Balozi Mpungwe nami nikaona nitie langu kumuunga mkono lakini si leo bali kurejea nyuma miaka mingi sana nikiwa na umri wa miaka 15 mwanafuzi wa sekondari:

Ujumbe mzito.

Nashukuru mimi niliyajua haya ya uwezo wa akina mama miaka mingi sana nyuma nina umri wa miaka 15 na ninae shahidi hapa barzani mwanamme mwenzangu wa kunisadikisha.

Shahidi wangu Chief Edward Makwaia.

St. Joseph's Convent mimi na Ted tulikuwa darasa moja form 1 D na hili darasa tulichanganywa wanawake na wanaume.

A na B wanaume watupu na C wanawake watupu.

Darasani kwetu form 1 D tulikuwa na wasichana wakitutesa sana katika masomo na nawakumbuka hadi leo: Salma na Radhia Bhatia mapacha hawa, Asya Kharusi, Sambayawo Nyirenda (hawa walikuja kuwa madaktari) na Jagjit Singh.

Nimemsahau katika wanafunzi ''extremely intelligent'' - Gulamabbas Jivraj.
Nimemkumbuka baada ya kumuona hapo kwenye picha ni huyo wa kwanza kushoto waliosimama.

Hatari kubwa sana.

Anaefuata ni Israel sikumbuki jina lake la pili tulikuwa tunakaa pamoja darasani na nje ya darasa kivuli changu akinipenda sana.

Baba yake ndiyo alikuwa Balozi wa Israel Tanzania.

Huyu alikuwa rafiki yangu sana lakini alinitesa mno wakati wa ''Six Day War,'' akinipa taarifa zote asubuhi nini kimetokea wakati wa vita vile.

Jeshi la Israel liliingia ndani ya Misri wakateka ''radar,'' wakaenda nayo Israel.

Jamaa ananihadithia with ''glee,'' hajui kuwa rafiki yake naungua maini.

Aliondoka shule baada ya Tanzania kuvunja uhusiano na Israel kwa ajili ya vile vita wakarudi kwao.

Nilifika Barlev Line, Sinai upande wa Misri nikiangalia nikiwa Suez Canal mwaka wa 1988.

Huu ni mpaka wa mlima mkubwa wa mchanga walioweka Wayahudi Sinai kujikinga, ikanikumbusha huyu sahib wangu na ''War Communique,'' zake tukiwa shule.

Wengine siwakumbuki majina.
''Last but one,'' waliosimama ni mimi.

Waliochutama kulia ni Edward Makwaia, anaefuata kati ya hawa mapacha wawili Salma na Radhia Bhatia ni Asya Kharusi (hadi tunamaliza shule sikuweza kuwatambua yupi ni yupi).

Angalia walivyofanana katikati yao ni Asya Kharusi, Iddi Mvule (alikwenda kusoma Economics Soviet Union akauliwa huko), David Gabba, waliobaki siwakumbuki.
Lakini na sisi wanaume tulikuwa na wakali wetu "vipanga" wetu wakitoa ushindani mkali sana - Ted mwenyewe, William Mfuko, David Gabba, Iqbal Bapumia na Charles Mesquita huyu alikuwa hatari amehifadhi hadi log.

Kwa hiyo hili la uwezo wa akina mama nililijua mapema sana.
Nilitaka kuwasahau walimu wetu ambao wataishi ndani ya nyoyo zetu siku zote.

Ajabu ni kuwa wote hao ni wanawake.

Headmistress Sister Jacinta, waalimu wetu Sister Gerda, Mrs. Grant (wengine majina nimeyasahau), Mrs. De Souza, Miss Menez huyu mwalimu wangu wa Literature kanijaza Shakespeare na Wole Soyinka akanisimamia siku ya mtihani wa Oral English kiti chake kaweka sawasawa na mimi na kila ninapojibu swali naona anatabasamu.

Kanikazia macho.
Alikuwa anasisitiza darasani umuhimu wa ''correct pronunciation,'' na ''contruction.''

Na kasema kwa wale wanafunzi wake wa ''Litereture,'' hakubali kingine isipokuwa Merit, Pass.

Hawa walimu walitokaga wapi?
Inatosha.

Screenshot_20220309-171351_Facebook.jpg
 
Duh! waqt umekwenda sana maalim wangu ila tunafarijika kuwa na wakongwe kama wewe humu maana mji bila wazee ni vurugu tupu.ah sitaki kuandika mengi nikaonekana kama na bonga hakuna tabia siipendi kama ya wazulu inayoitwa kubonga yaani kusifia kitu kuliko kusifia kitu kupita kiasi. Nitoshe kusema unatufaa sana kwa kumbukumbu na ilmu nyingi unayotupa hapa.
 
Duh! waqt umekwenda sana maalim wangu ila tunafarijika kuwa na wakongwe kama wewe humu maana mji bila wazee ni vurugu tupu.ah sitaki kuandika mengi nikaonekana kama na bonga hakuna tabia siipendi kama ya wazulu inayoitwa kubonga yaani kusifia kitu kuliko kusifia kitu kupita kiasi. Nitoshe kusema unatufaa sana kwa kumbukumbu na ilmu nyingi unayotupa hapa.
Guasa...
Huyo Allan Quarterman...
Rider Haggard.

Iko siku natembea milimani Edinburgh Castle nikakuta kibao kinaonyesha pub ambayo Rider Haggard akipenda kukaa na kuandika vitabu vyake.
 
Umekumbusha shule yangu ya vidudu
St joseph.... Nmemkumbuka sister salvina

Ova
Mrangi,
Ile ilikuwa shule.

Ikitokea fursa nitakuwekea hapa mambo mazuri niliyopitia St. Joseph's na watu ambao nilisomanao na nikaja kukutananao baadae sana ukubwani mbali mno na nyumbani.
 
Back
Top Bottom