CHOTABUSARA
Member
- Feb 6, 2012
- 47
- 48
Ni vyema kuwashukuru na kuwapongeza mama zetu kwa kutulea toka tumboni mpaka leo. Watu husema wababa wengi hufa mapema kuliko wamama kutokana na kutokuongea na hivyo kupata magonjwa yatokanayo na misongo ya mawazo.
Jana ilikua siku ya wanawake duniani, wanawake wengi waliongelea ubora wao na jitihada katika kazi, wamesifiwa na watoto wao wa kiume na wa kike, utasikia huyu anasema mama aliuza maandazi ili kunisomesha mpaka nikamaliza, huyu anasema mama aliuza pombe za kienyeji ili nisome nk.
Kwa sababu hii ya wanawake kubarikiwa kuongea na kutokana na hali halisi na maumbile mama huwa karibu zaidi na watoto, ni kama ambavyo jogoo hatembei na vifaranga, watoto hawa hushawishiwa kuwa mama yao amehangaika sana kuwalea kuliko baba yao na hii huwafanya watoto hawa wanapokua watu wazima kuelekeza mapenzi mengi zaidi kwa mama kuliko kwa baba.
Lakini nani atawasemea wababa wale wanaolala baharini na maziwani ili kuvua na kupata kipato kwa ajili ya familia zao, nani atawasemea wababa wale walio chini ya migodi na wakati mwingine kufia huko wakitafuta kwa ajili ya familia zao, na bahati nzuri baba akipata furaha inaongezeka katika familia, yaani baba atalea mama na watoto,
Tatizo kubwa huwa kipato kikizidi baba ataongeza mpenzi wa pembeni lakini bado nia ni kusambaza furaha, wamama wengi wakipata kipato kikubwa ndio chanzo wa kuvunjika kwa ndoa, huwa wanasema ndoa ya nini naweza kulea watoto wangu, mwanaume wa nini kama ninamudu maisha yangu, ni ngumu sana ndoa kuendelea kama mama ana kipato zaidi ya baba labda baba awe tayari kwa fedhea zote.
Wanaume inabidi kutafuta jinsi ya kuonyesha jitihada na umuhimu wetu kwenye jamii, na hii tabia iliozuka ya mwanamke kusifiwa sababu tu kapata nafasi fulani hata kabla hajafanya lolote haiwajengi bali inawafanya watukuze zaidi uwanamke wao, ili tutaliongea siku nyingine.
Nani atawasemea wababa wanaopandisha zege gorofa ya kumi kwa ajili ya familia zao, wale waliolala chini ya magari na mitambo mikubwa (mafundi) kwa ajili ya familia zao, wanaokesha wakiendesha ndege, meli, magari moshi, mabasi, taxi, dala dala nk. kwa ajili ya familia zao, wapiga Debe, madalali, waliopo maofisini na viwandani kwa ajili ya familia zao nani atawasemea.
Leo hii Ukraine wababa wameambiwa wabaki kupigania nchi yao, watoto wako na mama zao wanakimbia nchi, watoto wale wataambiwa na mama zao nakupenda mwanangu tutakufa wote, Nani atawasemea waliobaki wanapishana na mabomu na wengi watakufa
Kama wanaume hatukubarikiwa kuongea itafutwe jinsi ya kuonyesha jitihada zetu pia katika familia na jamii.
MWANAUME