Siku ya wanawake duniani/siku ya wanawake Tanzania: Nyange binti Chande wa Tabora

Siku ya wanawake duniani/siku ya wanawake Tanzania: Nyange binti Chande wa Tabora

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
SIKU YA WANAWAKE DUNIANI/SIKU YA WANAWAKE TANZANIA

NYANGE BINT CHANDE MWANAMAMA ALIYEJITOLEA NYUMBA YAKE KUWA OFISI YA TANU KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA

Kuna mtu alipata kusema kuwa utafika wakati watoto na wajukuu wa wapigania uhuru wataingia katika makabati na masanduku ya wazee wao kutaka kuimarisha historia za wazee wao waliopigania uhuru wa Tanganyika.

Leo nimepokea picha ya Bi. Nyange bint Chande mmoja wa akina mama waliokuwa mstari wa mbele katika TANU Tabora.

Bi. Nyange alijitolea nyumba yake kuwa ofisi ya TANU.

Vyama vya akinamama - Nujum ul Azhar, Waridatil Hubb na Egyptian Club vilivyokuwapo mjini Tabora chini ya Bi. Nyange binti Chande na Zarula binti Abdulrahman vilisaidia sana kuipa TANU nguvu katika Jimbo la Magharibi.

Tanzania ina deni kubwa sana kwa hawa wazalendo.

1678256241251.jpeg

Nyange bint Chande
 
Back
Top Bottom