Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!”

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,
Leo asubuhi nimeangalia kipindi cha mahojiano ya Makamo wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumzia Siku ya Wanawake Duniani kwenye TBC akihojiwa na Shabani Kissu.

Kwa Waliosikiliza kipindi hiki, kiukweli huyu ni mwanamke wa kupigiwa mfano, mtanisamehe sina maneno ya Kiswahili ya kujitosheleza kumuelezea, she is just so womanly, so genuine, so simple, very humble na down to earth!, ana a very rare charisma, which is very hard to find kwa viongozi wetu wengi wa kisasa. Kwa jinsi alivyo na sauti safi, tamu na laini yenye lafudhi ya Kizanzibari, akiongea, utatamani asimalize kuongea, utatamani aendelee tuu kuongea, ukijumlisha na yale macho...!, sijui hata akitaka kugomba, atagomba kwa sauti gani na macho gani maana...!.

She is just everything a woman needs to be!. Ingekuwa ni amri yangu ningetaka wanawake wenye uongozi, madaraka na mamlaka waige mfano wa Mwanamke huyu and to be honest I wish if Mungu angemua, huyu mama ndio akawa, then amini usiamini tutakuwa na Tanzania nzuri 100 times kuliko Tanzania hii tulionayo sasa!.

On Womanliness
Akizungumzia kuhusu mwanamke kushika madaraka ya juu kama yeye, akasema uongozi ni utumishi wa watu, haijalishi jinsia yako bali kuwatumikia watu hivyo ukiishajitambua kuwatumikia watu, wewe ni mtumishi wa watu, unapaswa kujituma kwa bidii na kuwatumikia watu hao kwa uaminifu, uadilifu na unyenyekevu wa hali ya juu lakini bila kujisahau uanamke wako kwa sababu kazi ya uumbaji kati ya mwanaume na mwanamke ni kazi ya Mungu, hivyo haijalishi wewe ni nani, bali mwanamke atastahili kujikubali uanamke wake na kujiheshimu kianamke kwa sababu mwanamke siku zote ataendelea kuwa mwanamke kwanza hayo mengine yote yanafuata.

On Simplicity and Down to Earth.
Amesema toka kuteuliwa kuwa Makamo wa rais, ana miss sana baadhi ya mambo ya wanawake mfano anapenda sana kupika na haswa kusukuma chapati. Lakini kutakana na kutingwa na majukumu, hapati tena muda wa kuingia jikoni kupika!. Wanawake wa Kizanzibari, wanapenda kwenda shopping ile kutembea tuu toka duka moja hadi jingine na kuchakura na kuchagua kuna raha zake. Tangu amekuwa VC anatamani sana kwenda madukani kuchakura, lakini anakatazwa. Anaulizwa aseme chochote anachotaka wako watu watatumwa kumletea.

On Humility
Akiongea na Kisu anaongea kwa unyenyekevu sana, haonyeshi kujisikia, anazungumza kwa tone ya humility ya hali ya juu. Angekuwa mwingine kwa madaraka aliyo nayo angeongea very authoritatively kwa tambo, majigambo na full kujisikia!.

Huyu Mama ana Virtues karibu zote na baadhi yake ni hizi nilizozitaja humu.
Ingekuwa ni amri yangu, ningemwambia tuu naniliu aamue 2020 asigombee his second term, na badala yake, ampishe ili awe huyu mama!.

Mungu ambariki sana Mama Samia na kuwabariki wanawake wote leo siku ya Wanawake Duniani.

Paskali
 
Ni kweli mkuu ni vizuri tuwaheshimu na kuwapenda mama zetu, pia tuwatie moyo na kuwaunga mkono kwa manufaa ya nchi yetu
 
kingereza cha nini?
 
Umean dika vizuri ila Nimekuja kusoma jina la mtoa Mada, Duuuuu ndg yake Dev, walewale
 
Pasco Pasco Pasco ( Pascal Mayalla) ndugu yangu bado tunahitaji ji mchango wako katika Hili jukwaa . Hili jukwaa ni chombo pekee huru katika nchi hii. Kauli yako hii "to be honest I wish if Mungu angemua, huyu mama ndio akawa, then amini usiamini tutakuwa na Tanzania nzuri 100 times kuliko Tanzania hii tulionayo sasa!."" nadhani utatuchoshea jopo letu la mawakili Maana limetumia miezi minne kumpatia Mh LEMA dhamana .kwa ndoto yake ya kuwa RAIS atakufa . Sasa Na wewe unawish Mungu ANGEMUA!
Halafu umesahau akisimama Makonda sorry BASHITE amesimama....... au unawish Mungu gani? Huyu akisimama BASHITE ? Ikiwa ni Huyu Unadhani BASHITE atakubali?
 
Mkuu Hivi punde , huu ndio Utanzania, Undugu, Utu na ubinaadamu, Mungu ambariki sana huyu mama.

Yaani huyu balozi wetu Dr. Pindi Chana, she used to be a very confident lady, sijui confidence yake imepotelea wapi hadi kushindwa kumtembelea Lissu siku zote hizi, lazima Balozi ajisikie aibu, yeye yuko Nairobi kumtembelea Mtanzania, Mbunge, Rais wake wa TLS (Pindi ni Lawyer), Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, ni mpaka VP aje ndipo na yeye aende kumuona Lissu!.

All and all, better late than never.

Wamefanya uungwana mkubwa.

Paskali.
 
Mkuu Paskali nimesoma hii post kwa makini na hakika nimeamua niiptint then niitumie kama mizani ya kujipima ninavoongoza watu hata kwa level ya familia. A masterpiece Mkuu. VP ni mama, you just see it from her face
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…