Wanabodi,
Leo asubuhi nimeangalia kipindi cha mahojiano ya Makamo wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumzia Siku ya Wanawake Duniani kwenye TBC akihojiwa na Shabani Kissu.
Kwa Waliosikiliza kipindi hiki, kiukweli huyu ni mwanamke wa kupigiwa mfano, mtanisamehe sina maneno ya Kiswahili ya kujitosheleza kumuelezea, she is just so womanly, so genuine, so simple, very humble na down to earth!, ana a very rare charisma, which is very hard to find kwa viongozi wetu wengi wa kisasa. Kwa jinsi alivyo na sauti safi, tamu na laini yenye lafudhi ya Kizanzibari, akiongea, utatamani asimalize kuongea, utatamani aendelee tuu kuongea, ukijumlisha na yale macho...!, sijui hata akitaka kugomba, atagomba kwa sauti gani na macho gani maana...!.
She is just everything a woman needs to be!. Ingekuwa ni amri yangu ningetaka wanawake wenye uongozi, madaraka na mamlaka waige mfano wa Mwanamke huyu and to be honest I wish if Mungu angemua, huyu mama ndio akawa, then amini usiamini tutakuwa na Tanzania nzuri 100 times kuliko Tanzania hii tulionayo sasa!.
On Womanliness
Akizungumzia kuhusu mwanamke kushika madaraka ya juu kama yeye, akasema uongozi ni utumishi wa watu, haijalishi jinsia yako bali kuwatumikia watu hivyo ukiishajitambua kuwatumikia watu, wewe ni mtumishi wa watu, unapaswa kujituma kwa bidii na kuwatumikia watu hao kwa uaminifu, uadilifu na unyenyekevu wa hali ya juu lakini bila kujisahau uanamke wako kwa sababu kazi ya uumbaji kati ya mwanaume na mwanamke ni kazi ya Mungu, hivyo haijalishi wewe ni nani, bali mwanamke atastahili kujikubali uanamke wake na kujiheshimu kianamke kwa sababu mwanamke siku zote ataendelea kuwa mwanamke kwanza hayo mengine yote yanafuata.
On Simplicity and Down to Earth.
Amesema toka kuteuliwa kuwa Makamo wa rais, ana miss sana baadhi ya mambo ya wanawake mfano anapenda sana kupika na haswa kusukuma chapati. Lakini kutakana na kutingwa na majukumu, hapati tena muda wa kuingia jikoni kupika!. Wanawake wa Kizanzibari, wanapenda kwenda shopping ile kutembea tuu toka duka moja hadi jingine na kuchakura na kuchagua kuna raha zake. Tangu amekuwa VC anatamani sana kwenda madukani kuchakura, lakini anakatazwa. Anaulizwa aseme chochote anachotaka wako watu watatumwa kumletea.
On Humility
Akiongea na Kisu anaongea kwa unyenyekevu sana, haonyeshi kujisikia, anazungumza kwa tone ya humility ya hali ya juu. Angekuwa mwingine kwa madaraka aliyo nayo angeongea very authoritatively kwa tambo, majigambo na full kujisikia!.
Huyu Mama ana Virtues karibu zote na baadhi yake ni hizi nilizozitaja humu.
Ingekuwa ni amri yangu, ningemwambia tuu naniliu aamue 2020 asigombee his second term, na badala yake, ampishe ili awe huyu mama!.
Mungu ambariki sana Mama Samia na kuwabariki wanawake wote leo siku ya Wanawake Duniani.
Paskali