Mkuu
Pascal Mayalla , hivi Form two hukusoma topic ya summarization/ paraphrasing?
Nyingi ya threads zangu ni makala za magazetini, nina 1/2 page Nipashe ya Jumapili na Mwananchi ya Jumatano, kazi ya mwandishi ni kuandika tuu, summarization na paraphrasing ni kazi ya chief sub editor, ila mimi by nature ni story teller, na ni mwana fasihi, hivyo baadhi ya threads zangu haswa za mambo magumu, napiga mastory marefu to drive home my point kwa kudunga sindano za taratibu, ukifanya short and clear, ukidunga sindano, utasababisha maumivu!. Ila pia nina mabandiko kibao tuu mafupi.
Hoja za bandiko hili ni nyingi, hakuna summary.
Nimesema, japo kikatiba binadamu wote ni sswa lakini kuna watu hawakubali kutawaliwa na mwanamke, fursa ilipojitokeza, wakafanya siri, wakamtuma Tanga wafanye mambo, wakashindwa!.
CCM bado haijawa tayari kumshindanisha mgombea urais kwa mchakato wa ndani ya chama, ndipo zikapigwa zile sarakasi za Dodoma.
Na October, tunapomchagua rais Mwanamke, tumpe na wabunge wanawake na madiwani wanawake, kisha tuvifute viti maalum.
P