Pre GE2025 Siku ya Wanawake Duniani: Wanawake acheni kubwetekea kubebwa. Viti Maalumu ni kubebwa

Pre GE2025 Siku ya Wanawake Duniani: Wanawake acheni kubwetekea kubebwa. Viti Maalumu ni kubebwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Viti maalumu ndio njia pekee waliyobakiza , kupambana majukwaani ni wachache sana wanaweza hiyo.
Viti maakumu vikifutwa itawalazim wapambane
Kwa vile mwaka huu, Watanzania wanakwenda kumchagua rais mwanamke, wanawake wakijitokeza kwa wingi kugombea, tutawachagua na tukiisha fikisha idadi ya 50/50, then kunakuwa hakuna haja ya viti maalum, tunavifuta, na kushindana kwa usawa.
P
 
Mkuu Pascal Mayalla , hivi Form two hukusoma topic ya summarization/ paraphrasing?
Nyingi ya threads zangu ni makala za magazetini, nina 1/2 page Nipashe ya Jumapili na Mwananchi ya Jumatano, kazi ya mwandishi ni kuandika tuu, summarization na paraphrasing ni kazi ya chief sub editor, ila mimi by nature ni story teller, na ni mwana fasihi, hivyo baadhi ya threads zangu haswa za mambo magumu, napiga mastory marefu to drive home my point kwa kudunga sindano za taratibu, ukifanya short and clear, ukidunga sindano, utasababisha maumivu!. Ila pia nina mabandiko kibao tuu mafupi.

Hoja za bandiko hili ni nyingi, hakuna summary.
Nimesema, japo kikatiba binadamu wote ni sswa lakini kuna watu hawakubali kutawaliwa na mwanamke, fursa ilipojitokeza, wakafanya siri, wakamtuma Tanga wafanye mambo, wakashindwa!.
CCM bado haijawa tayari kumshindanisha mgombea urais kwa mchakato wa ndani ya chama, ndipo zikapigwa zile sarakasi za Dodoma.
Na October, tunapomchagua rais Mwanamke, tumpe na wabunge wanawake na madiwani wanawake, kisha tuvifute viti maalum.

P
 
Pascal, unasemaje juu ya wanawake waliopata fursa kuwanyanyua ambao hawana..kwa nini kauli mbiu isiwe pedi kwa wote na maternity servies burepia kwa shule hostel kwa wote...kwa sasa women are more in indecent activities than before
 
Back
Top Bottom