Siku yako ya kwanza kupima UKIMWI, ulikuwa katika hali gani?

Siku yako ya kwanza kupima UKIMWI, ulikuwa katika hali gani?

Isingekuwa nimepima mpk Leo
Ilitokea tu nimepata shida kwenye mguu nikaenda kabla hata hawajaniijia badala Yule daktari sijui nesi ashughulikie mguu wangu ye akaanza kuniambia maswala ya kupima!!
Nikamwangalia nikaona isiwe tabu pima mama..!
Akaanza kutoa sijui ndo nasaha sijui ushauri mi ndo kwanza natabasam! Ikabidi nayeye aangue kicheko maana aliona jitu lenyewe analolihubiria ndo kwanza linatoa mitabasam halina hata wasiwasi..
Akaona afate kipimo tu apime kuliko kuendelea na nasaha zake.
Komamanga nikatolewa damu ikawekwa kwenye kipimo Sasa hapo kidogo ndo nikawa serious na tumapigo twa moyo tukaongezeka baada ya kujiuliza hivi njia ya maambukizi si moja tu ati uzinzi tu hata kiwembe kinatosha.. hivyo unaweza usiwe mzinzi ila kiwembe tu kikatosha kukulapua..😅😅
Kahofu kaliniongezeka halafu ubovu kipimo dada Yule akawa amekiacha mbele yangu naona tu damu yangu inavyoparangana hata sielewi ikienda wapi ndo nitakuwa imo..😂😂

Bahati nzuri baada ya muda akaja akaniambia nipo gud mwake mwake ndo akanishughulikia kilichokuwa kimenipeleka!!

Namsifu na kumlaumu isingekuwa yeye mpk leo nisingekuwa nimepima na maswala ya kupima watu Mambo ambayo hawaja yafwata aache kutiana mi presha tu..😂😂

Sasa Kuna Kobe nilivyoisimulia nayenyewe siku ya siku ikajitosa ikifikiri ile Kama sehemu ya kwenda kujitambulisha na kuondoka..😂
Bahati nzuri nae alitoka hana ila kwa kimbembe alinipigia simu baada ya kutoka tu.. vitu vyengine sio vya kuiga..
 
Njia ya kuambukiza ukimwi ni moja tu? Hata nilipopima mara ya mwisho miaka mitatu iliyopita nilikuwa bado bikra ila hofu haiwezi kukosekana lazima itakuwepo walau kidogo
Watu wamekariri japo elimu hutolewa mashuleni na vyombo mbalimbali vya habari.
 
Halafu siku hizi mbona hawatoi hata ushauri nasaha? Mimi mara ya mwisho kupima nilienda tu hospitali na ishu zangu tena sikuwa hata naumwa nilitaka tu kutega kazini. Kufika nikamwambia Dr naumwa kichwa... akaniuliza mara ya mwisho kupima VVU lini nikamwambia miaka 10 iliyopita, kaniandikia nikaenda kupima...hata wakati wa kutoa majibu wala hakuwa na maelezo yoyote.
Sjajua ulipoenda utaribu upoje ila Mara nyingi lazima kaushauri na maswali ya kuhoji yawepo kabla na baada ya kupima
 
Back
Top Bottom