Siku Yanga ikipoteza mechi, mashabiki wa Yanga wataingia uwanjani

Siku Yanga ikipoteza mechi, mashabiki wa Yanga wataingia uwanjani

Cosovo

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2018
Posts
667
Reaction score
1,810
Kwamba Yanga ikipoteza mechi hata moja ,itapoteza mwelekeo,na mashabiki watapaniki ,wachezaji watacheza kwa presha kubwa

Au nyie mnasemaje?
IMG_20220102_102426.jpg
 
Yanga wanacheza maigizo ya soka,na wanaweza kufanikiwa kucheza maigizo kama haya hadi wakachukua ubingwa.

Tatizo ni mechi za kimataifa tu.Huwa ni vigumu kucheza maigizo huko.Ndio maana huwa hawafiki mbali.
Bado hawajaamua kucheza mpira.
 
Kwa takwimu za Tff msimu uliopita Yanga ifungwa marambili na alikosea ubingwa, Simba alikua Bingwa na alifika makundi kwenye mashindano ya CAF Ila takwimu zinaonyesha Yanga iliongoza kwa mashabiki wake kuingia viwanjani ao ni Tff wanao simamia Soka la Bongo.
Yanga ndio timu ya Wananchi, Hakuna Shabiki wa mpira katika nchi hii asiye na Asili ya Yanga kwakua bila Yanga kusingekua na Uhuru katika nchi hii.
Kiasili Yanga imeshiriki kwa namna moja au nyingine katika ukombozi wa nchi nyingi kusini mwa Bara la Africa. Yanga ni maisha ya mtanzania, utake usitake Ulazimwishi Ila ndio ukweli. Muulize Baba yako au Babu yako kwenye ukoo wao Kuna Yanga wangapi alafu utapata jibu tunajadili Nini.
 
Hahahaaa. Naona mmeanzisha uzi wa kujifariji. Lol

#Mkishaamka msisahau kupiga mswaki.
Yaani mashabiki wa simba ni changamoto! Wameanzisha uzi wao wa kujitekenya na kujichekesha, huku wananchi tukiwachora tu 🙄

Sasa kwa Yanga ya msimu huu, kweli kuna shabiki wa kumtafuta mchawi kweli iwapo timu itafungwa? Na hiyo timu ya kuifunga yanga ipo kweli?

Binafsi tangu usajili wa awali ulipofanyika (achilia mbali huu wa dirisha dogo unao endelea), naamini Bingwa wa Ligi Kuu msimu huu ni Yanga!

NB: Nawausia Wachezaji kuendelea kutoa vipigo mwanzo mwisho, ili hawa mbumbumbu fc wakose cha kusema mwishoni mwa msimu! Safari hii hakuna kabisa kucheka na Kima.
 
Nawaaminia wachezaji. Unakumbuka ule msako prisons waliotembezewa baada ya kupata goli, na biashara alivosachiwa mpaka akakubali kutoa.

Juzi Dodoma walitaka kuleta dharau wakapigwa kipigo kizito.

Kuna wale watoto wa kitanga naskia wanajitapa huko, ngoja tuone itakuaje.

Na mapolisi huko Moshi naskia wanapiga gwaride kukamia.

All in all makolo wasiwatwishe wenzao mzigo uliowashinda. Wawe wapole.
 
Back
Top Bottom