Siku za mwisho za Saddam Hussein na Maombolezo ya askari wa Marekani

Siku za mwisho za Saddam Hussein na Maombolezo ya askari wa Marekani

Ertugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
14,705
Reaction score
30,041
Screenshot_20260728-170050_Chrome.jpg


Ndo ile ukisikia adui yako kawa rafiki yako ndio hii sasa,

Baghdad, Iraq

Ni wanajeshi 12 miongoni mwa askari 551 amboa walijulikana kama "Super twelve' walipewa jukumu la kumlinda raisi Saddam Hussein mwisho mwisho wa uhI wake kabla hajanyongwa

Mmoja wao Barden Werper ameandika kitabu "Mfungwa ndani ya kasri lake,Walinzi wake wa Kimarekani na kile ambacho historia ilikiacha bila kusema"

20260728_154040.jpg


Barden anakiri kwamba wakati anamkabidhi Saddam kwa wale walio kuwa wanakaribia kumnyonga,wanajeshi wote walio kuwa wanamlinda walilengwa na machozi

Wanajeshi hao wanasema hawakumuona Saddam kama muuaji katili bali walimuona kama babu yao.

Saddam alishitakiwa mahakamani kwa kuamuru mauaji ya wapinzani wake 148.

Siku zake za mwisho gerezani alipenda kusikiliza nyimbo za Mary J Blidge mwanamuziki wa Marekani. Alipenda kuendesha baiskeli ya mazoezi ya mwili ambayo alikuwa Akiita "Pony"


View: https://youtu.be/8XNaPX6MKlU?si=ndyBCg5-hP-9HG-w


Alikuwa anapenda sana kula pipi na keki ndogo aina ya Muffin.

Saddam alipenda kuvuta sigara aina ya " Cohiba" aliyemfundisha kuvuta ni homeboy Fidel Castro

Mwamba alikuwa mwangalifu sana na chakula chake,alikuwa anatengeneza kifungua kinywa chake kwa awamu. Kwanza mayai ya kukaanga,halafu keki na mwisho matunda. Iwapo mayai akiona yamekatika katika basi anayaacha na kutayarisha mengine.

Wakati mmoja Saddam aliwaambia hommies ambao ni walinzi wake kwamba alisikitika sana na kitendo kilichofanywa na mwanae Uday. Huyu homeboy mpuuzi alifyatua risasi mbele ya kundi kubwa la watu ambao walikuwa kwenye sherehe na kuua kadhaa na kujeruhi kadhaa,hapa utaona kwamba watoto wa namba moja wote huwa na akili sawa.

Saddam anasema alichukia sana na kuamuru matoyi ya homeboy Uday yachomwe moto zikiwemo Rolls-Royce, Ferrari na Porsch na kushuhuda miale ya moto ikitoka kwenye kwenya magari hayo.

Mmoja wa walinzi wake wa Kimarekani,alimtaarifu Saddam kwamba kafiwa na kaka yake,basi Saddam akamwambia yule homeboy kuanzia leo mimi nitakuwa Kaka yako,walitengeneza bond kubwa sana na mwamba Saddam.

20260728_154410.jpg


Usiku mmoja mmoja wa walinzi hao 12 wa Saddam alionekana kavaa suti kubwa sana iliyomfunika karibia mwili mzima, wenzake wakaanza kumcheka,ikaja kubainika kwamba alipewa suti hiyo kama zawadi na Saddam.

Urafiki uliendelea kushamiri kati ya Saddam na walinzi wake kadri ya siku zilivyo zidi kwenda,ingawa walipewa maagizo kwamba wasiwe karibu na Saddam Hussein.

Barden anasema hatukumpa Saddam Zaidi ya alichostahili ila hatukuumiza utu wake.

Steve Hutchinson ,ChrisTasker na walinzi wengine walijaribu kubadilisha chumba cha dawa na kuwa kama ofisi ya Saddam

Lengo la yote haya ilikuwa ni kubadilisha au kujaribu kutengeneza mazingira ya gereza yawe kama ofisi ya kiongozi wa Serikali kwa ajili ya Saddam

Mara tu alipoingia kwa mara ya kwanza askari alikimbia haraka kwenye meza na kufuta vumbi,Saddam aliona ishara hii na kutabasamu akikaa kwenye kiti.

Saddam alitengenezewa mazingira kama vile mahakama ni yake. Barden anasema askari walijaribu kwa uwezo wao kumfanya Saddam awe na furaha. Kwa upande wa Saddam yeye alikuwa anacheka na kutaniana nao na kufanya mazingira hayo kuwa ya furaha.

Baadae askari mmoja alimwambia Barden werper wanaona kwamba kama kuna jambo likiwatokea basi huenda Saddam anaweza kuhatarisha maisha yake kwa ajili yao

Kila Saddam alipopata nafasi aliwaomba kumlinda pamoja na familia yake.

Sehemu iliyo washangaza wengi kwenye kitabu hiki ni ile ambayo,inaelezwa kuwa askari hao walioomboleza kifo cha Saddam,walichukuliwa kama maadui wakubwa wa Marekani.

Adam Rigerson mmoja wa askari hawa alimueleza Barden werper kwamba baada ya Saddam kunyongwa,waliona kama wamemsaliti

"Tulijiona kama sie ndio wauaji wake. Tuliona tumemuua mtu ambaye alikuwa karibu yetu

Baada ya Saddam kunyongwa mwili wake ulitolewa nje na watu wakaanza kuutemea mate na kumdhihaki.

Mmoja wa askari hawa baada Saddam kunyongwa alijiuzuru nafasi yake ndani ya jeshi la Marekani.

Upendo ndio kila kitu kwenye maisha,walio kaa na Saddam walipata kumjua kwa upande wa pili wa utu wake.

Saddam alikuwa na matumaini kwamba hadi siku yake ya mwisho kwamba asingenyongwa

Disemba 30,2006,Saddam aliamshwa saa 9 siku

Dakika chache kabla ya kunyongwa alimwita Steve Hutchinson aliyekuwa nje ya Seli na kumpatia saa yake aina ya "Raymond Well"

Hutchinson alipotaka kukataa ,Saddam alimlazimisha na kupokea. Mpaka leo saa hiyo ipo inafanya kazi kwenye nyumba ya Hutchinson huko Goba/Georgia.

Ni hayo tu!
 
..hili ni funzo kwa Watawala Makatili.

..simulizi hii inaonyesha jinsi Saddam Hussein alivyokuwa akijutia aliyoyafanya.

..bila shaka aliyafanya yote hayo akitumaini ataepuka kitanzi.

..zaidi alitaka aage dunia akiwa ametenda mambo mema, ndio maana akawa mkarimu kwa walinzi wake.

..Saddam alitaka hii hadhithi kumhusu yeye itoke wakati atakapokuwa hayuko duniani.

..Kwa kifupi Saddam alikuwa katika kipindi cha TAFAKURI, MAJUTO, na IBADA.
 
..hili ni funzo kwa Watawala Makatili.

..simulizi hii inaonyesha jinsi Saddam Hussein alivyokuwa akijutia aliyoyafanya.

..bila shaka aliyafanya yote hayo akitumaini ataepuka kitanzi.

..zaidi alitaka aage dunia akiwa ametenda mambo mema, ndio maana akawa mkarimu kwa walinzi wake.

..Saddam alitaka hii hadhithi kumhusu yeye itoke wakati atakapokuwa hayuko duniani.

..Kwa kifupi Saddam alikuwa katika kipindi cha TAFAKURI, MAJUTO, na IBADA.
Kama ulishawahi kumkamata jambazi au kibaka halafu mkamgusa kichapo kidogo huwa wanatia huruma sana kuonyesha majuto, ila huwa ni uoga wa kuona kifo mbele yake anatamani muda urudi nyuma ajisafishe hicho ndiyo kilimpata alhaj Saddam Hussein
 
Back
Top Bottom