Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Kuna mdada mmoja anataka talaka kwa kuwa wenzake au mashosti zake wanaishi vizuri,hivyo kumpeleka kuona kwamba majani ya bustani za wenzake ni yakijani sana kuliko ya kwake
Anasema mume wake kila baada ya wiki mbili hununua vyakula vyote vya ndani,na kisha kila siku huacha shilingi elfu saba [7,000] za kununua mboga,lakini anasema hela hiyo haitoshi kwakuwa akinunua bando basi hela hubakia kidogo sana
Kama haitoshi mwanamke huyu anazidi kuhamasishwa na mama yake eti ahachike kwa mume huyo mbakhiri ambaye maisha ya mwanaye mabaya kuliko ya mashosti zake
Wakati huo huo kuna wanawake ambao kila siku wanaachiwa elfu tano [5,000] tu na hakuna kitu chochote ndani,na maisha yanenda hivyo hivyo,je huyo anayenunuliwa vitu ndani na kisha kuachiwa elfu saba daily na huyu ambaye hanunuliwi vitu ndani na kuachiwa elfu tano yupi ana maisha mazuri?
Inasemwa hivi siku zote ukiyaona maisha ya watu wengine unaweza kuona wanafaidi sana au wana unafuu sana lakini lau ukiyajua maisha yao kiundani zaidi utashangazwa sana
Binafsi nimewahi shuhudia maisha ya jirani yangu mmoja ambaye alikuwa na usafiri wake lkn inafikia kipindi gari huko inaisha mafuta na kuomba msaada kwa watu gari ipate kufika nyumbani,na si mara moja ni mara nyingi,lkn ukimuona ndani ya gari utasema maisha si ndio haya
Huu ni mfano mmoja,lakini kuna watu ambao maisha yao ni ya kuigiza waonekane mambo safi lakini wamejawa na madeni chungu nzima,nyumba haina amani kwa kudaiwa lkn mbele za watu wanaonekana mbele ya watu
Sasa kwakuwa huyajui maisha ya watu kiundani unajikuta unatamani kuwa kama wao lau ungejua ukweli wa maisha yao ungejiona wewe una maisha mazuri sana
Ndio mfano wa huyo bibie,anaona wenzake wanaishi vizuri lakini hajui undani halisi wa maisha yao,yupo radhi apewe talaka akakae nyumbani kuliko kuwa katika ndoa ambayo kwa mtazamo wake hana maisha mazuri
Tusiwe watu wenye kutamani maisha ya watu wengine,kwani hakika hatujui undani wa mambo yao,istoshe hata kama ni kweli wapo vizuri kumbuka hayo ni maisha yao na si yako,ridhika na maisha yako huku ukipambana kuwa bora zaidi
Ni hayo tu!