Sikuabliani na Magufuli kuhusu somo la Historia. Kama ni Uzalendo, watoto watajifunza kwenye somo la URAIA

tatizo lako ni uelewa, nimekuuliza uniambia umepata faida gani kuwasoma hao ili kujustify kelele zenu kuwa kuwafundisha watoto historia ya tanzania ndio kuwafanya wawe wazalendo
Una matatizo ya kuelewa wewe.Nimekujibu hao hawasomwi wanatajwa kwa sehemu ndogo sana.Alafu hata utoe povu hapa utobadilisha chochote na mwanao atasoma.Kama hutaki hama nchi.
 
Uzalendo haufundishwi darasani mkuu
 
2015 tulifanya makosa makubwa sana! Na hii itatugharimu! Yaan mtu mmoja kwa matakwa yake mwenyewe anatuharibia elimu yetu na hakuna wakumzuia!
 
Miaka 100 ijayo kuna jamaa ataingizwa kwenye list ya madikteta maana kila kitu kipo waz ni swala la mda tu
 
Uzalendo haufundishwi darasani mkuu
Sawa mkuu!Ila historia inafundisha watu kuwa wazalendo.Pia Historia inabeba utamaduni wetu na ndio utu wetu.Tusipowafundisha watoto wetu Historia yao watajivunia ya wengine huko ndiko kujipeleka utumwani kifikra.Ila alichokosea hiyo Historia ya Tanzania kufanya somo linalojitegemea hii ni kuongeza mzigo kwa watoto wetu.Ingeunganishwa na Uraia au History inayofundishwa Sasa.
 
Hata hivyo yeye mwenyewe Magufuli siyo mzalendo, unless BAKITA wawe wamebadili tafsiri ya neno Uzalendo kwenye kamusi. Angekuwa mzalendo asingerundika Taasisi za kimkoa na kikanda kijijijni kwake Chato.

Wala asingeua uchumi kwa kuwabambikia matajiri makesi na kuwadhulumu fedha zao
 
Hili somo litakua si somo la Historia ya Tanzania ni somo maalumu la kukaririsha watoto wa Tanzania kuhusu Magufuli na miradi yake iliyokufa...nothing else
Swadaktaaaaaa! Yaani ndiyo nia yake huyu mpenda sifa.
 
Somo jipya la historia nadhani syllabus zake zitakuwa..

*Jinsi Mfalme Magufuli alipoikomboa Danganyika 2015

*Mfalme wa Chato alipoifanya danganyika kuwa 'donakantre' duniani.
 
Ni lipi uliwahi kumpinga Rais zaidi ya kutukuza, elewa kuwa hatuwez kuwa na mawazo sawa kwa nchi nzima
 
Miaka 100 ijayo kuna jamaa ataingizwa kwenye list ya madikteta maana kila kitu kipo waz ni swala la mda tu
Nitafurahi sana kama hata hiyo historia itaandika ukweli kuhusu udikteta wa huyu nduli
 
Kwani somo la historia si linafundishwa miaka yote? Why this unnecessary emphasise?
 
Somo jipya la historia nadhani syllabus zake zitakuwa..

*Jinsi Mfalme Magufuli alipoikomboa Danganyika 2015

*Mfalme wa Chato alipoifanya danganyika kuwa 'donakantre' duniani.
Na kingine itakuwa "mbuga ya Burigi ilianzishwa na ......mwaka.....
 
Ndalichako amsema Historia ya Tanzania itafundishwa kwa shule zote sambamba na somo la historia linalofundishwa kwa sasa. Sasa kama somo husikatayari linafundishwa kuna haja gani ya ku-duplicate efforts na content? Ni wazi kuwa kufundishwa masomo mawili yanayofanana kwa wakati mmoja kuna kitu kinatafutwa, tena kwa udi na uvumba. Kukumbuwa kuwa Msumva wa Chato aliukwaa urais akafufua ATCL na menguneyo, basi. Anaingiza taifa kwenye ghara zisizokuwa za lazima kwa lengo la kujikweza na kujinufaisha binafsi!
 
kuna mambo ya maana ya kupewa msisitizo kwenye elimu lakini sio upumbavu HISTORIA, yaani awamu imewafanya watanzania wawe wajinga zaidi na wasiotambua wanataka nini.
Ngoja niachane na huu ujinga nienda kuangalia mechi
 
Mm nimesoma arts. Unaweza ukaniambia hapa nistory paper 11 Advance inatufundisha lolote cc kama wata? Au ni yaleyale sheria zinafundishwa kwa kingereza af hukumu ziandikwe kwa kiswahili???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…