Sikuamini nilivyofika Njombe, kumbe Tanzania hii kuna sehemu kama hizi?

Kwani ukilima Mbeya lazima usafurishe mzigo kwenda Kilimanjaro?
sio lazima hio nimetolea mfano maana mwanzisha mada ni mzawa wa huko ila ata Ndani ya mkoa kuvuka wilaya lazima ukute kibao CHA SIMAMA UKAGULIWE, WAKALA WA MISITU
 
Challenge hiyo hasa KUCHOMEWA MAENEO ya hizo TAASISI waisemeaje kiongozi
Inadaiwa kwamba wao ndiyo walikuwa wanaratibu hiyo michezo kwa ajili ya kuwaandalia maeneo hao wawekezaji.
Kule ardhi inakuwa ni ya kijiji sasa kuna watu wanamili ardhi kimila na ukiomba wakuuzie wanakataa kwasababu ni eneo la vizazi na vizazi; Kuondoa hiyo changamoto ya kunyang'anya ardhi viongozi wanaamua kuchoma moto tu ili kesho uliueze kwa bei mbaya. Utakula hasara pale unapokuwa umepanda miti.

Kinachofanya watu wastuke ni kwamba viongozi wengi wakubwa wa awamu ya nne wana mashamba makubwa sana eneo lile lakini moto huwa haufiki kwenye mashamba yao hata siku moja.

Kuja siku Mzee moja kiongozi wa kijiji kile ndiyo akanisumulia ambavyo watu huwa wanatumwa kuratibu huo uharibifu. Nikaishia kusikitika tu....Wao ndiyo wahusika hivyo sidhani kama wanaweza kusaidia chochote kile
 
Kwa kweli umenishawishi niangalie kwa ukaribu yaani ni neema tupu
Ila acha niweke na tupicha maana watu tunapenda uhalisia zaidi kuliko maandishi pekee
Na shingopana waliishi huko miaka mingi iliyopita
Yaani huko umenishawishi niende likizo
 
Ukanda huo umebarikiwa sana, ujue kuna sehemu zina Ardhi nzr kiasi kwamba zikitumika vzr lazma mafanikio yawepo, unaaenda sehem kipindi kama hiki cha kiangazi unakuta mimea yote ya Kijani but wazawa ni masikini

Nabaki na maswali mengi sana
 
Nenda mkuu , najua hutarudi iv iv unaweza kufanya kitu kwa ajili ya watoto wako
 
Tuna kawimbo ketu watu wa njombe na upangwa. Kanaenda


Upangwa\njombe nchii nzuri kuliko Zote,mashamba na bustaani twalima soote twachunga ngombe zeetu huu mlimani,ni nani ajuaaye uzuri wake huo huooo huooo huko huooo njombe\upangwa nitakaa

Karibu khinyumba kaka
 
Lasway.Jr ni kweli kabisa, njombe ni eneo limebarikiwa sana kwa ardhi nzuri na hali ya hewa, nilikuwepo hapo september kuangalia uwezekano wa kuwaunganisha wakulima wa viazi shirika langu la Agriterra unaweza kuangalia (agriterra.org) tukishirikiana na SAGCOT
 
Nenda mkuu , najua hutarudi iv iv unaweza kufanya kitu kwa ajili ya watoto wako
Napenda sana sehemu kama hizo, ingawa niko mbali sana na nyumbani lakini naomba Mungu retirement yangu iwe sehemu nzuri kama hiyo
 
nimekumiss Lasway.Jr !yeah huko njombe nchi ya asali nami nimefika jaman ni kuzuri maparachichi na mazaga zaga kibao yanastawi vizuri mnooooo ! safi sana kwa kazi yako aisee !sema mbali duh
Asante, mbali mbinguni, uwekezaji ni popote , tamani siku moja watoto wako waje waseme baba/mama aliona mbali sana haaa haaa you must have your children brain for bow for them
 
Asante , pia Unaweza kuangalia , www.greenagricultureskills.com
Uone kazi zetu
 
Juzi Rais alisema, kuzaliwa Tanzania ni fursa. Watu wakaanza kumponda
Ilinikera siku moja nikiwa kwa hao ndugu zetu, kijana mmoja akaniuliza "kwa nini Tanzania ni miongoni mwa nchi masikini sana duniani wakati mna raslimali nyingi" nilikereka sana! Nikamwambia kuwa Madini ya Tanzanite kwa mfano huwa yanapatikana Tanzania tu! Nikafungua site hii: http://allafrica.com/stories/201405120444.html na hii Tanzanite Gemstone in Jaipur, Rajasthan | tanzanite stone Suppliers, Dealers & Retailers in Jaipur hakunighasi tena
 
Bila shaka hicho ni kijiji cha madeke mkuu...
 
Mkuu lupembe nmetoka juzi tu kijiji kinaitwa mfiriga so mchezo ardhi kule ina rutuba so mchezo mi nlienda kutafuta mashamba ya kupanda miti ya mbao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…