Sikuamini nilivyofika Njombe, kumbe Tanzania hii kuna sehemu kama hizi?

Sikuamini nilivyofika Njombe, kumbe Tanzania hii kuna sehemu kama hizi?

kutoa mzigo hapo mbea mpk Kilimanjaro unakutana na wakala wangap wa misitu huko barabarani na ni hela kiasi gani utawaachia
alafu pili refer wakulima wa mbaazi utajua kwa nn watu wengi wanalima kwa mitego mitego
Boss ulipogusia issue ya Mbaazi umenigusa vibaya mno kama mie mwaka jana nilinunua mbegu elfu5 kwa Kg nimejaribu kulima tu 2acres nnakuja sokoni nnaambiwa 1kg Tshs 150-300 na tena kwa sasa hawazihitaji maana zimejaa tele
 
Boss ulipogusia issue ya Mbaazi umenigusa vibaya mno kama mie mwaka jana nilinunua mbegu elfu5 kwa Kg nimejaribu kulima tu 2acres nnakuja sokoni nnaambiwa 1kg Tshs 150-300 na tena kwa sasa hawazihitaji maana zimejaa tele
pole mkuu shida ya Tanzania siasa za chuki na visasi ndo zinatangulizwa mbele angalia mambo mengi sana wanakurupuka angalia issues ya kupeleka maindi kenye.
Mkuu nikushauri kitu kama unauwezo wa kuyasafirisha bora utafute shele zilizopo mkoa mingine uwauzie wao wayatumie kama maarage
 
Mkuu yaan watu km nyie huwa mna ni motivate sana endelea kutueleza fursa zilizopo kwenye kilimo .
 
Katika mizunguko yangu ya kazi nilitoka Morogoro nikaenda Mbeya kufanya shughuli zangu za kilimo hasa umwagiliaji, basi nikiwa Mbeya pale kwa kuwa mimi ni mdadisi nitampigia jamaa yangu mmoja ambae ni mwenyeji wa Mbeya pia ni Mkulima, duh jamaa mcheshi sana na ni mshikaji sana japokuwa ni msomi mkubwa na mfanyabiashara

Basi akanambia njoo huku Njombe,jioni ile nikapanda gari kuelekea huko, nilipofika nikakutana na jamaa ang mmoja niliesoma nae chuo akanipokea na akawa mwenyeji wangu.
Nilipompigia jamaa angu huyu Mkulima akanambia bado hajafika mjini ndio anatoka shamba, kumbuka hapo ni saa nne usiku.

Kesho yapo ikawa asubh , baridi ilikuwa kiasi japokuwa mwenyeji wangu alinambia ni wakati wa joto kwa sasa haaa haaaa Njombe kama ulaya vile

Kama saa moja hivi jamaa angu alikuja akanichukua , tukampitia na mshikaji wake mmoja , na safari ikaanza ya kuelekea nisikokujua kwenye nchi ya maziwa na Asali kama Mwendo wa 80km tukaanza kukwepana na milima ya Lupembe na baada ya muda mshikaji wangu akanambia hapa ndio tunaingia shamba, kwa kuwa lilikuwa shamba jipya lenye milima na milima , na lilikuwa Shamba kubwa kiasi , haaa haaa sio kubwa kama unavyofikiria ww ila ni zaidi ya hekari 400+ Virgin land , hapo hapo nikaanza udadisi wangu na kuanza kukumbuka nilivyokuwa nafundishwa na Maprofesa wangu enzi hizo nasoma pale SUA ,

Nilichoshangaa ni nn?
Katika udadisi wangu niligundua kuwa ile Ardhi haikuwahi kulimwa , mimea iliyoota maeneo Yale iliashiria rutuba ya ajabu iliyoko katika udongo ule , hali ya hewa na baadhi ya vitu vilionyesha kuwa eneo lile linapata mvua kubwa sana kwa mwaka tatribani 2300mm per yr
f8e30fe5a8f17a71a09ce3f3cca203a6.jpg


Organic matter layer ya Ardhi ile ni zaidi 40cm,
Nilichoshangaa zaidi ni pale nilipoenda ndani ya Shamba zaidi na kuona kuwa kuna chanzo kizuri cha maji , nilitamani niende kwetu Rombo niwachukue wale wazee niwalete pale kwa sababu kule sijawahi kuona kitu kama kile .
Bhasi nikaendelea na utafiti wangu nikagundua vitu vingi zaidi katika Ardhi ile na baada ya kukaa na kuangalia milima ikishangaa ujio wetu na muda ulikuwa umeenda , tukafanya baadhi ya kazi pale na kuanza kurudi

Ninachotaka kusema ni kwamba
Don't limit your mind to think
Seed and not diamond will make Africa great
Wekeza vzr kwenye kilimo
Uzi utakao fuata nitawaeleza katika hyo Ardhi ni nini kimepandwa na kinawezaje kumlipa Mkulima tena bila stress , najua utafikiri ni miti ya mbao lakini sio kweli ....stay tuned
Jumapili njema wana jamvi
Mtoto wa Mzee Mmari, kila siku unani inspire ... Thanks bro ..
 
Mtoa mada yuko sawa, na wachangiaji wako vzr, kinachonikwaza ni soko kutokuwa huru, wakulima wengi wanamahindi maghalani bei bado iko chini mno, pesa ya kulimia wengine wamekopa na wanamahitaji mengine kama ada za watoto achilia mbali ununuzi wa pembejea kwa msimu utakaofuata, nini kifanyike? kwa maoni yangu serikali iruhusu kuuza mahindi nje hususani kenya ni soko zuri hii itapandisha bei ya mahindi na wakulima hususani kizazi kipya watahamasika kulima na itapunguza joto la ajira, wakubwa kumbukeni tuko ndani ya jumuiya ya Afrika mashariki na law of comperative advantage kwa hili iko upande wetu.
 
Sema tunapana vikumbo na makampuni makubwa kama New Forest na wale wa One Acre Fund. Wanamiliki maeneo makubwa sana na Raisi Kikwete aliwapa tu;


Wananchi waliuza mashamba yao wenyewe. Kama umemsikia mheshimiwa Mwamoto (mbunge) amebaini kasoro mbalimbali ikiwemo kutopitia Kituo cha uwekezaji (TIC) ukisema kikwete aliwapa tu, yawezekana hujafanya utafiti wakutosha.
 
Mkuu Njombe cha mtoto sana mimi nafanya kilimo sehemu moja inaitwa Kidabaga iko Iringa huko. Ni balaa sana na hali ya hewa ni kama Ulaya, zamani Mahindi walikuwa hawapandii mbolea.

Sema tunapana vikumbo na makampuni makubwa kama New Forest na wale wa One Acre Fund. Wanamiliki maeneo makubwa sana na Raisi Kikwete aliwapa tu; Inafika kipindi wananyanyasa wazawa na kuchoma mashamba yao ya miti kwa maksudi pindi ukikataa kuwauzia.

Nawashauri vijana watembee na kuwekeza huko. It is a nice place to invest: jaribu kwenda kufanya utafiti mkuu

NB: Kuna vibarua wengi sana wa bei nafuu na Wahehe wengi ni watu waaminifu sana endapo utawapa stahiki zao kwa wakati.
Nimekaa sana madege pale kariakoo, huko kilolo ni pazuri pia
 
Bangi ya Njombe siyo kali sana kama ya Arusha maana huko baridi si kali sana!
Makinda anaielewa sana...
Kuna pahala Mbeya panaitwa Rungwe broo, mwaka mzima ni kijani. Vyanzo vya maji kibao
 
Back
Top Bottom