Sikuamini nilivyofika Njombe, kumbe Tanzania hii kuna sehemu kama hizi?

Kuna pahala Mbeya panaitwa Rungwe broo, mwaka mzima ni kijani. Vyanzo vya maji kibao
Ni kweli nako kuko vizuri nilifika kule kuna hawa jamaa wa gesi, nikafika kuna halmashauri mpya nimeisahau jina iko huko mbele ya Rungwe milimani
 
Umenikumbusha Kate, huko Sumbawanga , kuna watawa wa Benedictine wanakaa Abasia ya Mvimwa , wale jamaa wamewekeza kwenye kilimo hakuna mfano , maji ya kutosha , ardhi nzuri etc . Nilijifunza mengi sana kwa wale watawa aisee.
 
Ukanda huo umebarikiwa sana, ujue kuna sehemu zina Ardhi nzr kiasi kwamba zikitumika vzr lazma mafanikio yawepo, unaaenda sehem kipindi kama hiki cha kiangazi unakuta mimea yote ya Kijani but wazawa ni masikini

Nabaki na maswali mengi sana
Kama ukiwa na dhahabu kisha hauna akili bado ni ufukara tu
 
nimekumiss Lasway.Jr !yeah huko njombe nchi ya asali nami nimefika jaman ni kuzuri maparachichi na mazaga zaga kibao yanastawi vizuri mnooooo ! safi sana kwa kazi yako aisee !sema mbali duh
Hivi mpaka leo duniani kuna sehemu ni mbali?! Nadhani ni uwezo tu mdogo ila hakuna mbali. Wazungu wasingekuja huku kutubanabana
 
hayo ndo mambo ya msingi asee!! sio kila siku vijana kujadili mambo ambayo hayana hata faida kwetu, bado tuna ardhi kubwa ambayo ni idle, tutafuteni fursa popote ndani ya ardhi ya Tanzania yetu yenye amani na upendo.
Sure...kuna la kujifunza kwenye mijadala ya namna hii.
 
Very innocent and genuine comment.
Nahisi umewahi kujihusisha na uwekezaji ktk kilimo kwa jinsi ulivyo changia maoni yako.
Tembelea Makete uone jinsi tulivyobarikiwa kuku wanakula Apple's maana hakuna wakuzila,tunaomba mwekezaji atujengee kiwanda ili tusindike
 
Tembelea Makete uone jinsi tulivyobarikiwa kuku wanakula Apple's maana hakuna wakuzila,tunaomba mwekezaji atujengee kiwanda ili tusindike
Sasa mkuu kwanini usiweke kwenye maboksi, pakiza kwenye fuso uyalete huku Dar?
Utajiri huo mkuu.
 
Tembelea Makete uone jinsi tulivyobarikiwa kuku wanakula Apple's maana hakuna wakuzila,tunaomba mwekezaji atujengee kiwanda ili tusindike
Wewe uko makete? Apples mnalima varieties gani? Mimi nahitaji miche, naweza kupata huko?
 
Kwa mikoa niliyopita nadhani hakuna sehemu isiyofaa kwa kilimo

Kwa mfano watu wanasema singida kuna Ukame ila kuna maeneo kuanzia kinampanda kuelekea barabara inayokwenda hydom
Kuna ardhi kule siyo mchezo

Ukirudi Iringa nako ni balaa tupu

Njombe ndiyo usiulize,
Mbeya nako balaa kabisa

Pwani nayo japokuwa maeneo mengi yana maji ila bado panalimika

Morogoro huko ukipita mbingu katikati huko mpaka mgololo ni neema tupu.

Ukihitaji uwekezaji tenga bajeti ya kutembea
 
theoretical kilimo ni rahis na kinalipa mno
practical kilimo ni gamble nilikaa njombe nikaamua kujiingiza kwenye kilimo cha viazi aisee kama unategemea maisha yako yote mule utakufa na stress nashukuru nilikua mfanyakaz so nilikua nalima kutengeneza extra income misimu kama miwili nilikula hasara mpaka nikaja kukimudu haikua rahisi kama watu wanabohisi
pia nilikua na lecture wangu wa agriculture UD wa economics third watanielewa
alichukua heka za kutosha 100+ aliambulia hasara mpaka leo hana hamu na kilimo ingawa anafundisha hilo somo
 
Sasa mkuu kwanini usiweke kwenye maboksi, pakiza kwenye fuso uyalete huku Dar?
Utajiri huo mkuu.
Kwa kweli huku nilitembelea tu ila changamoto ni barabara ina bodi ziboreshwe ili at least wafanyabiashara waweze kukusanya
 
Mkuu salama,

Mbona hapo kama kijijini kwetu Mfiriga Lupembe, na juzi juzi lilipita doser likaangusha mti wangu pale kilimani, mbona kama ndio hapo? Hata hivyo, karibu sana kwetu Mfiriga.
 
Hali ya hewa ya njombe ni zaidi ya ulaya!ukanda ule wamebarikiwa sana
Wazee wa kulwenda kwao.mara mija kwa mwaka hata akae njimbe miaka mia atakwambia baridi lipo moshi huku hamna kitu,pesa ipo moshi huku hamna kitu ila ukimuuliza mbona hukubaki moshi atakwambia huku nimekuja kutafuta
Huwa hawaeleweki hawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…