Serikali angalia jambo hili usitafute mchawi kutoka mbali mchawi unaye hapo hapo ulipo kaa. Tazama, walimu waligoma ukawachapa ukasema warudi hataka madarasani vinginevyo utafuta ajira zao, wakaogopa, wakarudi haraka lakini mgomo wao ulibaki mioyoni mwao. Matokeo yake ndio haya. Taka usitake. Wengine wenye akili wakasema mbona huna mtaala rasmi? Kwa mbwembwe na madaha makubwa ukasema " nina mtaala kabambe na rasmi toka kitambo sana wasemao wote wana majungu" anguko hili limekuumbua kumbe huna lolote. Angalia sana ndugu yangu chukua hatua kabla hujachukuliwa hatua .
Nawasilisha