Sikubaliani na shambulizi la kimaudhui dhidi ya Dejan

Bila bila

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
22,168
Reaction score
39,118
Tàrehe 13.08.2022 kuanzia majira ya saa 3 usiku Kwa saa za Afrika mashariki, baada ya Mechi ya Ngao ya Jamii Kati ya Yanga na Simba, habari ya pili Kwa ukubwa baada ya habari ya matokeo ni underperformance ya mchezaji wa Simba raia wa Serbia Dejan Georgijevic.

Kumekuwa na maneno, maandishi na picha zilizofinyangwa zikionyesha si lolote si chochote. Sina shida na mashabiki wa kawaida àmbao utani na kuzodoana ni sehemu sahihi na Tamu kunogesha hitimisho la mchezo wa soka. Ninachopinga ni kitendo cha kumshambulia kibaguzi (mzunguuu) kunakofanywa na baadhi ya waandishi wa Habari na wachambuzi rasmi wa soka.

Ukiangalia kwenye kurasa za kina Shafii Dauda, Priva, Oscar, Gift nk utakutana na picha au maneno ya kejeli yakikosoa si performance yake mbovu tu bali yakiunganisha na race yake (Mzungu). Kitendo hiki kingefangika Uingereza Kwa Mbwana Samata (Aston Villa) kipindi kile waandishi na wachambuzi wa kitanzania wangetoa mapovu kulaani ubaguzi na kushambulia wazungu Kwa maneno kedekede.

Jambo hili kama linhefanywa na mashabiki wa kawaida ningeona poa tu lakini kufanywa na watu rasmi katika tasnia ya habari tena Kwa namna kubwa ya kejeli ya kibaguzi si maudhui Bora kiuandishi.

Mwandishi mmoja amefikia Kuweka video kwenye page yake ikimchambua Dejan kama "Mzungu wa Chalinze", mwingine kaweka video ilimwongelewa kama mwanaukoo wa Kocha wa Simba Zoran Maki ilimradi tu kudhalilisha Uzungu wake uonekane si Uzungu halisi ni Uzungupori.

Hii si Sawa ndugu waandishi na wachambuzi. Si Sawa kwenu kuwa Wazodoaji badala ya wachambuzi. Tunahitaji ukosoaji, lakini usihisishe udhalilishaji toka Kwa watu maalum kama nyie.

 
Hivi kumuita mtu mweupe mzungu ni ubaguzi?
 
Kama kuna watu wabaguzi, basi waafrika watakuwa wanaongoza halafu hawaoni hilo kama ni tatizo.
Sio haki wala sahihi kumkosoa kwa kukejeli asili ya rangi ya ngozi yake.
Uko sahihi. Na Sisi ndo Walalamikaji wa Kwanza tunapoguswa. Leo Samata akiwekwa mitandaoni na pembeni ikawekwa ndizi tutaongea mpaka Kiembesamaki watasikia.
 
Mkuu we ni MZUNGU? Kama "ndio" basi una haki ya kulia lia
 
Hivi kumuita mtu mweupe mzungu ni ubaguzi?
Inategemea Kwa nini umemwita hivyo. Mazingira ndiyo yana determine ubaguzi au sifa lakini hii ya Sasa ni pure ubaguzi na udhalilishaji. Hata Mtu mweusi kuitwa Mwafrika si tusi lakini linapotolewa Kwa namna dhalili linakuwa tusi.
 
Mleta mada huwezi kueleweka na wengi coz watu wengi wana fixed mind mentality kua kuitwa White au mzungu ni sifa,unakuta mtu akiitwa White anakua proud sana ila akiitwa black anatokwa povu,

Yaani mtu akiwa vizuri utasikia "Huyu jamaa ana mambo ya kizungu sana" ila mtu akiwa hovyo ataambiwa "Huyu ana mambo ya Kiswahili sana,huyu ana uswahili sana"
 
Mimi ni mshabiki wa simba, ila napenda tu kusema "lefa mzungu, leta mzungu, anajua huyo, anafunga huyo" 😂

Dejan ana viashiria vya kuwa mshambuliaji mzuri, ni kazi ya mwalimu kumuweka sawa kisaikolojia, kumjengea kujiamini ili aoneshe alichonacho mguuni, vinginevyo atafeli, na kufeli kwa mchezaji kwenye timu moja si ajabu, wameshafeli kina torres, kina sanchez, di maria tena hao WORLD CLASS PLAYERS
 
Uko sahihi. Na Sisi ndo Walalamikaji wa Kwanza tunapoguswa. Leo Samata akiwekwa mitandaoni na pembeni ikawekwa ndizi tutaongea mpaka Kiembesamaki watasikia.

Hivi naomba kuuliza hiyo ndizi unayosema ikiwekwa pembeni kwa picha ya Samatta maana yake ni nini?
 
Uko sahihi. Na Sisi ndo Walalamikaji wa Kwanza tunapoguswa. Leo Samata akiwekwa mitandaoni na pembeni ikawekwa ndizi tutaongea mpaka Kiembesamaki watasikia.
Kuwekwa ndizi hapo ni tatizo ila kumuita samata mweusi sioni tatizo hata kumuita dejan mzungu naona poa tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…