Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,168
- 39,118
Tàrehe 13.08.2022 kuanzia majira ya saa 3 usiku Kwa saa za Afrika mashariki, baada ya Mechi ya Ngao ya Jamii Kati ya Yanga na Simba, habari ya pili Kwa ukubwa baada ya habari ya matokeo ni underperformance ya mchezaji wa Simba raia wa Serbia Dejan Georgijevic.
Kumekuwa na maneno, maandishi na picha zilizofinyangwa zikionyesha si lolote si chochote. Sina shida na mashabiki wa kawaida àmbao utani na kuzodoana ni sehemu sahihi na Tamu kunogesha hitimisho la mchezo wa soka. Ninachopinga ni kitendo cha kumshambulia kibaguzi (mzunguuu) kunakofanywa na baadhi ya waandishi wa Habari na wachambuzi rasmi wa soka.
Ukiangalia kwenye kurasa za kina Shafii Dauda, Priva, Oscar, Gift nk utakutana na picha au maneno ya kejeli yakikosoa si performance yake mbovu tu bali yakiunganisha na race yake (Mzungu). Kitendo hiki kingefangika Uingereza Kwa Mbwana Samata (Aston Villa) kipindi kile waandishi na wachambuzi wa kitanzania wangetoa mapovu kulaani ubaguzi na kushambulia wazungu Kwa maneno kedekede.
Jambo hili kama linhefanywa na mashabiki wa kawaida ningeona poa tu lakini kufanywa na watu rasmi katika tasnia ya habari tena Kwa namna kubwa ya kejeli ya kibaguzi si maudhui Bora kiuandishi.
Mwandishi mmoja amefikia Kuweka video kwenye page yake ikimchambua Dejan kama "Mzungu wa Chalinze", mwingine kaweka video ilimwongelewa kama mwanaukoo wa Kocha wa Simba Zoran Maki ilimradi tu kudhalilisha Uzungu wake uonekane si Uzungu halisi ni Uzungupori.
Hii si Sawa ndugu waandishi na wachambuzi. Si Sawa kwenu kuwa Wazodoaji badala ya wachambuzi. Tunahitaji ukosoaji, lakini usihisishe udhalilishaji toka Kwa watu maalum kama nyie.