Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Kwanza ningependa kuendelea kutoa pole kwa wana CHADEMA kwa kifo cha kiongozi wao.najuwa kibinadamu inaumiza , kusikitisha,kuhuzunisha na kutia simanzi.
Lakini ningependa kusema ya kuwa tukio hilo lisifanye kupoteza imani kwa vyombo vyetu vya Ulinzi hususan jeshi la Polisi kama ambavyo tumesikia matamko yakitolewa na viongozi na Makada wa CHADEMA.
Ni wazi kuwa jeshi letu limepokea na kusikia sauti za watanzania wa vyama vyote na wasio na vyama namna walivyo laani na kukemea tukio hilo na ndio maana tumeshuhudia likiongeza nguvu ya timu nzito kutoka makao makuu kitengo cha upelelezi wa matukio makubwa.
Tumeona pia namna Rais wetu Samia Suluhu Hasssan alivyosikitishwa na kuhuzunishwa sana na kutoa amri ya kufanyika kwa uchunguzi wa kina na kupewa taarifa au ripoti juu ya suala hilo.
Lakini ningependa kusema kuwa unapokuwa kiongozi ni lazima na muhimu sana na busara kubwa sana kuchunga ulimi wako au maneno yako au kujizuia kuzungumza unapokuwa katika hali ya hasira,jazba au hali yoyote ile inayoweza kukufanya au kukuchochea kuzungumza jambo au kutoa tamko bila kufikiri zaidi ya kutumia hisia tu.
Ndio maana unapoitwa au kufikia hatua ya kuwa kiongozi ni lazima uwe na kifua,kujizuia kutanguliza hisia zaidi ,uchuje maneno,uwe na subira,utangulize hekima,busara na kuwa na Utulivu wakati wa nyakati ngumu zenye kila aina ya presha ya wafuasi wako au kwa sababu ya tukio fulani. Ni lazima uhakikishe ya kuwa unajizuia hisia zako katika kufanya maamuzi au kutoa maneno juu ya jambo fulani.
Sasa nimepita katika ukurasa wa Twitter wa Sugu mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Nyasa na kushangaa sana alicho kiandika. Kiukweli sikubaliani nacho kwa sababu kinaleta taharuki, uchochezi, uchonganishi na hofu kwa watu isiyo na ukweli. Ni maneno yanayoonyesha ameandika akiwa na hisia na kukosa utulivu au kufikiria kabla ya kuyaandika.
Kama kiongozi amekosea na amefanya kosa kubwa tu. Ameshindwa kujiongoza Mwenyewe na kutawala hisia zake na badala yake hisia zake zimemtawala na kumuongoza,jambo ambalo ni la hatari kwa kiongozi.Maana linakupunguzia ile nguvu ya kuitwa kiongozi Makini.
Maneno yenyewe na ujumbe wenyewe ni huu hapa.
PIA SOMA