Watu wengi wana mapenzi ya dhati kwa wazazi wao. Mapenzi haya bila shaka yanayokana na namna mzazi anavyotekeleza wajibu wake wa kulea familia aliyoanzisha. Mapenzi haya ya watoto kwa wazazi hayalazimishwi.
Mapenzi ya namna hii yanaweza pia kuwepo kwa wananchi kuipenda nchi yao pale viongozi wanapotekeleza wajibu wao wa kuendeleza nchi.
Kero zilizopo ambazo ni lazima zishughulikiwe:
1). Rushwa
2). Wizi wa mali za umma
3). Huduma hafifu za usambazaji maji, umeme, dawa, elimu bora, nk.
4). Miundombinu kwa upana wake
5). Makazi duni
6). Kupanda kwa bei za bidhaa
7). NK
Ni vyema kila mtu kuwajibika kwa nafasi yake. Hii ni pamoja na kuachia ngazi ikiwa mtu unaona mambo yamekushinda kusimamia au kufanya.
Kuna wizara ambazo kwa kweli ni shida sana. Miaka nenda, miaka rudi. Hadi karne hii ambayo kuna nchi zinaongelea jinsi ya kuweka makazi kwenye sayari zingine, sisi tunahangaika na maji ya kunywa, umeme, barabara, nk. Inatia huruma.
Tuipende nchi yetu, tuipambe kwa kila Kilicho kizuri zaidi.
Mungu walinde viongozi wetu
Wape hekima na busara
Waitendee mema nchi na wananchi
Usisite kulaani wote wanao tusababishia dhiki, shida.
Amina