Sikukuu za Krismasi za zamani ni tofauti na za sasa hivi

Sikukuu za Krismasi za zamani ni tofauti na za sasa hivi

VinJoe

Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
31
Reaction score
171
Nakumbuka zamani Christmas ilikua sikukuu kubwa kuliko hata mwaka mpya kwa familia yangu.. ilikua inasherehekewa kwa namna ya kipekee sana kwanza Christmas ilikua ni lazima siku hio mvua inyeshe so inakua na theme ya ubaridi mvua na matope. Lakini sidhani kama hio kitu bado ipo.

Zamani Christmas ilikua ni birthday ya Yesu ila ilikua kama ndio birthday yangu maana na nguo tutanunuliwa na midoli na vizawadi vyakitoto vyakutosha hapo kuna Uncle mmoja humkosi na vimfuko viwili vitatu vya pipi anatoa tu kila siku😂😂 ndugu mnakutana mnadherekea pamoja na hapo unakua na mizuka January ifike mfungue shule.

ILA SASA HIVI NATAMANI XMAS 🎄 IPITE HARAKA MAANA NI MIMI SASA ZAMU YANGU KUNUNUA ZILE ZAWADI NA KU SPOIL WATOTO NA VITU VIZURI VIZURI.

NA MASWALA YAKUKUTANA TENA SIO MUHIMU TENA KWA DUNIA HII YA LEO MAISHA YAKO SPEED KILA MTU ANAHISI AMEBANWA.. MAMBO YAMEKUA TOFAUTI SANA.

IBADA YA MKESHA WA XMAS ILIKUA MUHIMU SANA KWETU ILA KWASASA HATA SIJUI KAMA BADO HIZO IBADA ZINAFANYIKA ZAIDI NAJUA WAPI BATA ZURI LEO LIPO.
 
Dedication song, Hapo zamani,

Mr 2 Sugu na Mzee King Kii.

Maisha zamani yalikuwa mazuri ni enzi za Yo Rap bonanza.
 
Krisimasi ya zamani baada ya kula pilau na soda, mnapewa sh 50 au 100 ya kwenda kutembelea, kwa waliokulia Tabora wanapakumbuka Maua baa ndio tulikuwa tunaenda kuangalia video huko.......sio sasa hivi tunawapeleka kwenye ma beach kuogelea

Krisimasi ya zamani ilikuwa mnahamia kwa rafiki yake na baba na mkiwa huko habagui, wote tulikuwa tunanunuliwa nguo mpya, viatu vipya na ile miwani yenye fremu za njano........lakini sio sasa, huyohuyo rafiki yake baba anaweza kumbaka mtoto wa rafiki yake.
 
SIKUKUU NI KWA WATU WENYE PESA MKUU BILA HIVYO UTAISHIA KUSEMA SIO KAMA ZAMANI

TUWASHUKURU SANA WAZAZI WETU MAANA WALIZIFANYA SIKUKUU ZETU KUWA NZURI NA TAMU
Brother sijui kama nimeelewa point yako vizuri ila kaka sikukuu sio ya watu wenye hela tu kaka
Mimi kwenye kukua kwangu nili experience pande mbili za maisha.. kwa wazazi wangu familia zao kuna mmoja kwao zipo sana na mmoja kwao hazipo
Sasa labda nikuambia kwa upande ambao hazipo.. nilishawahi kwenda kwao kipindi cha sikukuu kaka watu wanashereekea kwa namna ya kipekee sana yaani kulingana na uwezo wao na wanasheerekea kweli.. kuna kitu kinaitwa super dip.. hii ni kama unga hivi inachanganywa na maji inakua kama juice. Sasa kwa uwezo wao watu wanachanganya hio super dip na watu wanakunywa wanaenjoy. Yaani ninachokumbuka inawezekana wale watu walikua wanafurahia sikukuu kuzidi wale walioko mijini au wale wakishua.

images (97).jpeg
 
Zamani zamani mambo yalikuwa poa, wajomba wakija home mnapewa Ela, siku hizi Kuna mjomba anayegawa hivyo, xmass wazaz wananunua kadi za kugawa kwa marafiki zenu, na wao wanawaletea mnapeana.
 
Zamani ilkua mwendo wa kusambaziana Mahot pot ya pilau tu[emoji23][emoji23] mtaa mzima unanukia pilau
 
Siku izi mjomba sindio wewe sasa kwanini hugawi ela mkuu..?[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Mi mjomba kwani,mi ke au me, wajomba wa Leo wachoyo kwa watoto wa Dada zao, mmoja wapo ukute wewe.
 
Kwani ma aunt hua hamna utaratibu wa kugawa ela?[emoji1]
Wajomba wananguvu kikwetu, mi nasemea wajomba wa zamani sio waleo, kwani we unasemaje? Hata ungekuwa karibu ningekujua ningekupa ya soda.
 
Hazina utofauti ni vile umekuwa Sasa, na hata watoto wa Sasa wakikua wataona utofauti, in short duniani hamna jipya
 
Back
Top Bottom