Rais wa nchi ana majumu makubwa ya kitaifa na kimataifa, si vyema kumsubiri aje atatue kila kero zilizoko nchini .Kufanya hivyo ni kumfedhehesha rais, na kudharau taasisi ya urais, rais apelekewe matatizo yaliyoshindikana kwenye ngazi zote za serikali.
Kama tutaenda namna hii tutajikuta tunaua mifumo yote ya usimamizi na kumtisha rais mzigo mzito ambao hatakaaweze kuubeba
Mwisho tutasimamisha na kurudisha nchi na taifa nyuma sana maana kila mtu atamsubiri rais.Tutaua ubunifu kwa viongozi wa chini katika kumsaidia rais kulitumikia taifa.Kuanzia mwenyekiti wa mtaa hadi mawaziri watamsubiri rais.
Hii itakuwa ni aibu kubwa sana kwa taifa lenye umri mkubwa namna hii kuua mifumo yake iliyojengwa kwa jasho na nguvu za wazalendo.Ingawa bado mifumo haijawa imara lakini angalau ipo inaweza kuimarishwa na kurekebishwa.
Tukatae mwenendo wa namna hii kwa nguvu zote maana haimsaidii rais wala taifa letu
Tusimshauri wala tusimbebeshe rais mzigo mzito hivyo. Tutarudisha nchi na taifa nyuma