Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Rostam Aziz alijiweka karibu na JPM akafanikiwa kuzindua Taifa gesi. Leo JPM hayupo anamdhalilisha kwamba alionga na utawala wake ulikuwa unaelekeza nini mahakama ifanye....kama kweli anachosema ndicho anachokiamini kwanini hakusema JPM akiwa hai? Kwanini hakuwahi kukemea?
Mwigulu ameonyesha dharau kwa kauli ya JPM kwamba matajiri wataishi kama mashetani. Lakini JPM huyo huyo ndiye anayemteua kuwa Waziri wa mambo ya ndani na baadaye kumrithi Mahiga; kama aliweza kuonyesha utii kwa JPM akiwa hai kwanini asimheshimu akiwa ameondoka?
Nimetoa mifano hii miwili kuwakumbusha viongozi wetu wakuu watatu kwamba wasiposimamia maadili na kuheshimiana baina ya wateule wao wajiandae kukabiliana na dhiaka kubwa wakiacha madaraka.
Haya yakiachwa yaendelee tukaamini uchawa ni dili katika karne hii hata wajukuu zetu kisasi kitawarudia. Hizi kauli zinaleta ufa mkubwa hasa ikizingatiwa JPM alikuwa na watu wanaomfuata bila unafiki na baadhi yao wapo wamejibanza kwenye regime iliyopo. Jiulizeni kama wafuasi wa JPM mnakula na kunywa nao huku mkimsema vibaya pamoja na heshima ya uteuzi aliyowapa mnaamini wanapata machungu kiasi gani?
Chukueni taadhari sana mnapoonyesha namna mlivyoishi na JPM kama rafiki kumbe miyoyoni mnamchukia. Inauma sana hasa linapofanywa na wale wale aliowaamini.
Ushauri wangu: Ficheni chuki zenu ndani msizitoe nje; mtukaneni kwenye vikao ndani ila mkitoka adharani mtunzieni heshima yake kama alivyowaheshimu ninyi. Naamini pamoja na makosa yake alikuwa na lengo zuri juu ya Tanzania; alijitoa katika Taifa lisilohitaji watu wa kujitoa. Amepumzika tumwache tuendelee pale alipoishia.